Habari za Punde

Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Kuzindua Mfumo wa Usajili wa Biashara Zanzibar.

Na.Kijakazi.Abdalla.    
Wizara ya Biashara na Viwanda na masoko  Zanzibar inatarajia kuzindua mfumo wa Usajili wa Biashara na amana kwa mali zinazohamishika kutumia mtandao wa komyuta.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Migombani Zanzibar Waziri wa Biashara ,Viwanda na Masoko Amina Salum Ali amesema kuwa mfumo huo wa usajili wa kutumia mtandao ni miongoni mwa matokeo ya jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar za kuhakikisha taratibu za uanzishaji na uendeshaji wa biashara Zanzibar unaimarika.
Alisema kuwa lengo la mfumo huo wa usajili biashara ni kurahisisha urasimishaji na uendeshaji wa biashara Zanzibar, kuwapunguzia gharama na muda wafanyabiashar na kupelekea kuvutiwa wawekezaji nchini .
Aidha Mhe, Amina alisema kuwa mfumo huo mpya utakuwa na faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuondokana na usumbufu nakupelekea  kuimarika upatikanaji wa huduma za usajili.
Pia alisema kuwa mpango huo utaimarisha  utunzaji wa kumbukumbu na upatikanaji wa taarifa za wateja pindi pale zinapohitajika.
Hata hivyo alisema kuwa mfumo huo wa usajili wa biashara utaimarisha mashirikiano miongoni mwa taasisi za kodi nazile taasisi nyengine zinazohusika na uanzishaji biashara kwakuwepo kituo kimoja cha usajili.
Uzinduzi huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 25/06/2018  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT,ALI Muhamed Shein ambae anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huko  katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil kikwajuni Mjini Unguja .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.