Habari za Punde

Mhe Mohammed Raza Atangaza Nia Kugombea Nafasi za Mwenyekiti wa ZFA Zanzibar

Mwakilishi wa jimbo la Uzini Mohammedraza Hassanal ametangaza nia ya kugombea Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kwa ajili ya kuliteka maendeleo ya mchezo huo.  
Raza ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari za michezo katika hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
Mwanamichezo huyo ambae aliwahi kuwa mshauri wa masuala ya michezo kwa Rais wa awamu ya tano Dk Salmin Amour, amesema nia hiyo imekuja baada ya kuona soka la Zanzibar kuanguka, hivyo ameona ipo haja kutangaza nia ili kuja kulikomboa.
Amesema atahakikisha anaukuza mchezo huo kwani atashirikiana ipasavyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo inaonekana ipo mstari wa mbele kwenye michezo.

ZFA watalazimika kufanya uchaguzi kufuatia viongozi wake wakuu kuamua kujiuzulu akiwemo aliyekuwa Rais Ravia Idarous Faina, Makamo Urais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali hivyo nafasi hizo mpaka sasa zipo tupu huku ikisubiriwa kamati ya Uchaguzi kutangaza tarehe za kuanza harakati za kufanyika uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.