Habari za Punde

Mchezo wa Ufunguzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Kati ya JKU na Zimamoto Uwanja wa Amaan.Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bao 2 - 2.

Wachezaji wa Timu ya Zimamoto wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya JKU kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Nane Bora wa Ufunguzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2. Katika Mchezo huo 
Bao la Timu ya JKU limepatikaka katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kupitia mshambuliaji wake Suweid Juma katika dakika ya 3 ya mchezo huo.
Zimamoto wamesawaszisha bao lao kupitia mshambuliaji wake Uwezo Jeremiah katika dakika ya 34 ya mchezo huo kipindi cha kwanza, hadi mapumziko timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili cha mchezo huo kimeaza kwa mchezo wa kushambulia kwa kushutikiza kila upande wakati wakiwa katika mchezo wa kutegeana kila upande katika dakika ya 56 ya mchezo huo kipindi cha pili Timu ya JKU imeandika bao la pili kupitia mshambuliaji wake Edward Peter. 

Zimamoto wakiwa katika mchezo safi na wa kujiamini sana wameweza kusawazisha katika kipindi cha pili cha mchezo huo katika dakika ya 65 kupitia mshambuliaji wake Hafidh Bakar. 
Hadi mchezo huo unamalizika Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2. 


Kikosi cha Timu ya Zimamoto kinachoshiriki michuano ya Nane Bora Ligi Kuu ya Zanzibar kilichoaza ufunguzi wa michuano hiyo na kulazimishwa kutoka sare ya bao 2-2. na Timu ya JKU katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kikosi cha Timu ya JKU kinachoshiriki michuano ya Nane Bora Ligi Kuu ya Zanzibar kilichoaza ufunguzi wa michuano hiyo na kulazimishwa kutoka sare ya bao 2-2. na Timu ya Zimamoto katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Nassor Mattar kushoto akimpita beki wa Timu ya Zimamoto Shafii Hassan wakati wamchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2. 
Wachezaji wa Timu ya JKU wakishangilia na kumpongeza mfungaji wa bao lao Mshambuliaji Suweid Juma alipoifungia timu yake katika dakika ya 3 ya mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Nassor Mattar akijiandaa kuzuiya mpira kumpita beki wa Timu ya Zimamoto Suleiman Said wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bara mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2.
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Nassor Mattar akimpita beki wa Timu ya Zimamoto Suleiman Said wakati wa nchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2. 
Wachezaji wa Timu ya JKU na Zimamnoto wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2.
Wachezaji wa Timu ya JKU wakimlalamikia muamuzi wa mchezo huo kwa mchezaji wao kuchezewa rafu kwa makusudi na mchezaji wa timu ya Zimamoto wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2.
Wachezaji wa Timu ya Zimamoto wakishangilia bao lao la kusawazisha lililofungwa na mchezaji Uwezo Jeremia katika dakika ya 34 ya mchezo huo kipindi cha kwanza.Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Salum Juma akijaribu kumpita beki wa Timu ya Zimamoto Yussuf Ramadhani, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2. 
Beki wa Timu ya Zimamoto kushoto Ali Salum na kulia mchezaji wa Timu ya JKU Suweid Juma wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 2-2.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.