NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso ameamuru kuwekwa ndani
wakandarasi wanaotekelezwa mradi wa maji yenye thamani ya zaidi ya
bilioni tatu eneo la mkata wilayani Handeni baada ya kushindwa kuwepo
kwenye eneo la mradi licha ya kupewa taarifa za uwepo wa ziara yake.
Wakandarasi ambao walilazimika kuwekwa ndani ni Mkandarasi wa Kampuni ya
Tansino Logistick Limited ya Dar Abdul Ismail na Charles Stephano
ambaye ni mkandarasi wa ujenzi huku Chales Tarimbo mshauri Mkandarasi
naye akikumbana na kadhia hiyo.
Agizo hilo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua
miradi ya maji inayotekelezwa kwenye kata ya Mkata wilayani Handeni
ambapo miradi hiyo mitatu ilikuwa ikigharimu zaidi ya sh.bilioni tatu.
Akiwa kwenye eneo hilo Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani wabunge
wanaomba miradi ya maji na serikali inatenga lakini watu wachache
wanatumia fedha hizo kwenye matumizi kwa maslahi yao binafasi na
kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka na tatizo la maji.
Alisema kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikirudisha
nyuma juhudi kubwa zinazofanywa serikali hawatavumiliwa badala yake
watahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha
vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.
“Ndugu zangu wakati Rais akiniteua aliniagiza nihakikisha wananchi
wanapata 1maji vinginevyo nitatumbuliwaa nami sipo tayari kwa hilo hivyo
nitahakikisha tunawachukulia hatua kali wakandarasi wanaoshindwa
kuendena na kasi na hivyo kuikwamisha kwa maslahi yao binafasi huku
wananchi wakiendelea kuteseka”Alisema.
Naye kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni
Mhita alimuelezwa Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo umejengwa chini ya
kiwango na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka na adha ya maji.
“Mh Naibu Waziri wilaya ya Handeni ni miongoni mwa wilaya ambazo
zinachangamoto kubwa ya tatizo la maji lakini sisi kama wabunge tumekuwa
tukiiomba fedha za mradi ya maji lakini wakandarasi wamekuwa
wakitukwamisha”alisema.
Alisema kinachofanywa na wakandasi hao juu ya utekelezaji wa miradi hii
ni ubadhirifu wa wazi kabisa hivyo ili kuondokana na tatizo hilo
serikali inapaswa kuwachukulia hatua wakandarasi wa namna hiyo ili iwe
fundisho wa wengine wenye tabia za namna hiyo.
Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema
miradi hiyo ambayo Rais aliagiza imalizike leo (jana)Julai 23 huku jambo
la kushangaza hakuna dalili ya umalizikaji wa miradi hiyo. Miradi hiyo
ambayo ilitakiwa kutelezwa Wilayani hapo ni pamoja na bwawa la
mkata,bwawa la manga na miundombinu ya mambomba toka katika bwawa la
mkata hadi mkata mjini jambo ambalo halijafanyika hadi mwisho wa agizo
No comments:
Post a Comment