Habari za Punde

Rais Dk Shein akutana na uongozi wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala BoraRais Dk. Shein alikutana na uongozi wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, chini ya Waziri wake Haroun Ali Suleiman ambaye katika maelezo yake ya utangulizi alieleza vipaumbele vilivyowekwa na Ofisi hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Mahkama Kuu Tunguu na jingo la Ofisi ya Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi.

Kipaumbele chengine alieleza kuwa ni pamoja na kuwezesha shughuli za Serikali na utoaji wa huduma kufanyika kielektroniki, kuendelea kutayarisha miongozo mbali mbali ya Utumishi wa Umma na kusimamia utekelezaji wake, kutekeleza program ya Mabadiliko katika Sekta ya Sheria na Mabadiliko ya  Utumishi wa Umma pamoja na kuimarisha usimamizi wa misingi ya Utawala Bora.

Nae Rais Dk. Shein wka upande wake aliupongeza uongozi wa Ofisi hiyo kwa kuendelea kutekeleza vyema kazi zake pamoja na kuwasilisha vyema utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Ofisi hiyo.
  
 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.