Habari za Punde

Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Timu ya Madaktari Bingwa Kutoka Nchini Brazil.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC}  Ofisini kwake Vuga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC}  Ofisini kwake Vuga.
Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC} Bwana Fabio Webber Tagliari  Kulia akiagana na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akibadilishana mawazo na Balozi Mteule wa Brazil anayetarajiwa kufanya kazi zake Visiwani Zanzibar mara baada ya kukamilisha  kwa Taratibu wa Kidiplomasia Nchini.
Afisa wa Mahusiano ya Kimataifa wa ABD Bibi Layana Coasle Alves Kulia akibadilishana mawazo na Balozi Seif  mara baara ya kumaliza mazungumzo yao Ofisini  kwake Vuga.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu wa Afya kutoka Nchini Brazil baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Ofisini kwake Vuga Zanzibar.(Picha na OMPR - Zanzibar)
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo haja ya kuendelezwa kwa Kamisheni ya pamoja kati ya Tanzania na Brazil itakayoratibu mashirikiano ya Kidiplomasia katika Nyanja za Kiuchumi, Historia na Maendeleo ikilenga kuimarisha ustawi wa Wananchi wa pande hizo mbili .
Alisema Tanzania na Brazil pia zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu katika masuala ya Utamaduni na Biashara unaopaswa kuendelezwa  kwa kuzingatia  kwamba ni Mataifa yanayofafana Kimaendeleo katika harakazi zao za kujiimarisha Kiuchumi.
Akizungumza na Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC}  Ofisini kwake Vuga Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Kamisheni ya pamoja kati ya pande hizo mbili ipo lakini kinachohitajika kwa sasa ni ufuatiliaji wa malengo iliyoazimia kuyatekeleza.
Balozi Seif alisema Zanzibar kwa upande wake inaweza kufaidika  na mpango huo kwa kujikita zaidi katika kufungua milango ya Ushirikiano na Nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kwenye Sekta za Biashara, Taaluma katika masuala ya kukabiliana na Maafa pamoja na huduma za Afya.
Aliueleza ujumbe huo wa Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC} ikiongozwa na Bwana Fabio Webber Tagliari  kwamba  Zanzibar hivi sasa inaendelea kuimarisha Sekta ya Afya kwa kuvijengea uwezo zaidi vitengo vinavyosimamia huduma za  Afya ya Mama na Mtoto.
Balozi Seif alifahamisha kwamba uamuzi wa  Taasisi hiyo  ya ABC kutoka Brazil ya kufanya ziara ya kuangalia uwajibikaji katika Sekta ya Afya Zanzibar  unakwenda sambamba na azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ya kuimarisha  huduma za Afya  katika umbali usiozidi Kilomita Tano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein Nchini Brazil katika kipindi kilichopita  imeanza kuleta faida kutokana na Nchi hiyo kushawishika na hatimae kuamua kufungua Ubalozi wake Mdogo Visiwani Zanzibar.
Alisema kwa hatua hiyo yenye muelekeo wa kukomaa kwa uhusiano wa pande hizo mbili milango ya Zanzibar iko wazi kwa Taasisi na Makampuni ya Brazil kuweza kuanzisha miradi yao ya Uwekezaji Zanzibar kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya Sekta ya Utalii.
Alieleza kwamba Brazil tayari imeshapiga hatua kubwa katika uendeshaji wa Sekta hiyo ya Utalii kiasi kwamba Taasisi  na Makampuni yake yanaweza kutanua Wigo wao wa Uwekezaji zaidi katika kulitumia soko la Zanzibar linalokamilisha Ujenzi wa Maegesho ya Ndege katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Aman Karume Zanzibar .
Naye kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Taasisi  inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Nchini Brazil {ABC} Bwana Fabio Webber Tagliari alisema Taasisi yao imeweka upendeleo Maalum wa kusaidia kutoa huduma za Afya Visiwani Zanzibar.
Bwana Fabio Webber alisema Wataalamu wake wamepanga kutembelea baadhi ya Hospitali na Vituo vya Afya kuona changamoto zilizomo na kuangalia namna Taasisi yao inavyoweza kusaidia nguvu za Kitaalamu katika Utoaji wa huduma za Afya ikiwemo Upasuaji.
Alisema Wataalamu na Madaktari hao wanafurahia  kuungana pamoja na Wataalamu pamoja na Madaktari Wazalendo katika kutoa huduma za Afya kwa Wananchi mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.