Habari za Punde

Mkutano wa Mashirikiano Kati ya Viongozi wa UAE na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) akisalimiana  na Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Reem Ibrahim Alhashimy alipofika katika viwanja  vya Park Hyatt Hotel kuungana na ujumbe wa timu ya Wataalam 16 wa Umoja wa Nchi za  Falme ya Kiarabu (UAE) uliofika Nchini kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibar aliyoifanya mwanzoni kwa Mwaka huu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) (wa pili kushoto) akiwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika kikao cha siku moja na Ujumbe wa  timu ya Wataalam 16 wa Umoja wa Nchi za  Falme ya Kiarabu (UAE) ukiongozwa na  Waziri wa Nchi Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bibi Reem Ibrahim Alhashimy (kulia) katika ukumbi wa mikutano wa Park Hyatt Hotel leo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) (wa pili kulia) akiwa na Viongozi Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd,Salum Maulid Salum,Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa Fedha na Uchumi Mhe.Mohamed Ramia Abdiwawa na Katibu wa Rais Nd,Haroub Shaibu Mussa, wakiwa katika kikao na Ujumbe wa  timu ya Wataalam 16 wa Umoja wa Nchi za  Falme ya Kiarabu (UAE) katika ukumbi wa mikutano wa Park Hyatt Hotel leo, [Picha na Ikulu.] 09/08/2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.