Habari za Punde

BALOZI STITH AHIMIZA KUENDELEZA USHIRIKIANO, AWAFAGILIA RAIS MSTAAFU MKAPA ,KIKWETE,MWINYI, ATUA BONGO KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA UBALOZI WAKE

Maraisi wastaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) Benjamini Mkapa (kulia) na Jakaya Kikwete (kushoto) kwa pamoja wakishiriki kukata keki na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Tanzania, kuanzia mwaka 1998 - 2001, Charles Stith (wa pili kulia) na mkewe, Debora Prothrow-Stith (wa pili kushoto) kukata Keki wakati wa hafla ya Balozi huyo kusherehekea kutimiza miaka 20 ya ubalozi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kempisk jijini Dar es Salaam jana
Maraisi wastaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) Benjamini Mkapa (wapili kulia) na Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) kwa pamoja wakifurahia baada ya kukata keki na Balozi Mstaafu wa Marekani nchini Tanzania, kuanzia mwaka 1998 - 2001, Charles Stith (wa tatu kulia) na mkewe, Debora Prothrow-Stith (wa tatu kushoto) wakati wa hafla ya Balozi huyo kusherehekea kutimiza miaka 20 ya ubalozi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kempisk jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mtoto wa balozi huyo,Mimi na (kushoto) ni mratibu wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Teddy Mapunda

 Balozi mstaafu wa Marekani nchini Tanzania, kuanzia mwaka 1998 - 2001, Charles Stith, akizungumza wakati wa hafla ya Balozi huyo kusherehekea kutimiza miaka 20 ya ubalozi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kempisk jijini Dar es Salaam jana
Rais mstaafu wa awamu ya nne,Jakaya Kikwete,akisalimiana na Balozi mstaafu wa Marekani nchini Tanzania, kuanzia mwaka 1998 - 2001, Charles Stith, wakati wa hafla ya Balozi huyo kusherehekea kutimiza miaka 20 ya ubalozi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kempisk jijini Dar es Salaam.
Balozi mstaafu Charle Stith na mkewe, Debora Prothrow-Stith wakicheza na msanii wa kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre,  wakati wa hafla ya Balozi huyo, kusherehekea kutimiza miaka 20 ya ubalozi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kempisk jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Safi Theatre, watoa burudani wa  wakati wa hafla ya Balozi mstaafu Charles Stith, kusherehekea kutimiza miaka 20 ya ubalozi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kempisk jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Muhidin Sufiani)    


Na Muhidin Sufiani
 ALIYEKUWA Balozi wa Marekani nchini Tanzania wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Benjamin Mkapa ,Balozi Charles Stith amesema anajisikia faraja kusherehekea miaka 20 ya ubalozi nchini kutokana na mapenzi mema na nchi ya Tanzania ambapo pia amekuwa akiendelea kusaidia katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo hapa nchini.

Balozi amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 20 ya ubalozi ambapo maraisi wastafu mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dk.Jakaya Kikwete walishiriki kwenye sherehe hiyo.

 Mbali ya marais wastaafu ,pia wakati wa sherehe hiyo viongozi wengine wa ngazi mbalimbali pamoja na wageni waalikwa wakiwamo baadhi ya madaktari bingwa kutoka Marekani pia  walishiriki.

Akizungumza wakati wa sherehe hizo Balozi Stith amesema akiwa balozi kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2001 amepata ushirikiano mkubwa kwa Rais mstaafu Mkapa huku Rais mstaafu Dk.Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Amemshukuru Mkapa na Kikwete kwa ushirikiano ambao walikuwa wakimpatia katika kuhakikisha uhusiano wa nchi hizo unaendelea na kwamba akiwa nchini Tanzania amefanikisha kuingiwa kwa makubaliano mbalimbali yenye tija kwa nchi za Afrika na hasa Tanzania.

"Nimefurahi kuja Tanzania kukutana na kusheherekea miaka 20 ya Ubalozi.Nimefurahi kumuona Rais mstaafu Mwinyi,Rais mstaafu Mkapa na Rais mstaafu Kikwete.Tulishirikiana na tunaendelea kushirikiana," amesema Balozi Stith.

Akizungumzia kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2001,Balozi Stith amesema kuwa akiwa Balozi ,alifanya mambo mengi ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana na Rais mstaafu.

Pia amesema wakati  akiwa nchini Tanzania alishiriki katika kutoa misaada mbalimbali ya kijamii na kwamba alishiriki kuhamasisha kampuni za Marekani kuja kushirikiana na kampuni za Tanzania.

Ameongeza kuwa akiwa Balozi amefanikiwa kufanikisha ujio wa viongozi wa ngazi za juu wa Marekani huku akieleza namna ambavyo alikuwa anatekeleza jukumu ambalo alipewa la kuandaa taarifa kuhusu namna Tanzania inavyopiga hatua kiuchmi.

Pia amesema akiwa nchini binti yake Mary-Mildred Stith(Mimi) anajivunia kwani alianza masomo yake nchini Tanzania katika Shule ya K
imataifa ya Tanganyika na kwamba kwa sasa ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu(PHD).

Amefafanua binti yake huyo anasoma Chuo Kikuu cha Boston nchini Marekani na Wasilisho lake la PHD linahusu maendeleo ya Tanzania.

Kwa upande wa marais wastaafu nchini nao wamepata nafasi ya kumzungumzia Balozi Stith na kwa sehemu.kubwa wamempongeza kwa namna ambavyo alitoa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo ya Tanzania.

Rais Mkapa amesema amefurahi kumuona Balozi Stith na kubwa zaidi anakumbuka.mchango wake wa kimaendeleo na changamoto zilizojitokeza wakati wa mlipuko wa bomu katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka ambao alianza kazi.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.