Habari za Punde

KATIBU MKUU UVCCM AWATAMBULISHA WAKUU WA IDARA WAPYA KWA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU UVCCM LEO.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) pamoja na wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walipowalisi katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya Makao Makuu UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl.Raymond Mwangwala (MNEC) akizungumza na watumishi wa Makao makuu wakati akiwatambulisha wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walioteuliwa na Kuthibitishwa na baraza kuu la UVCCM Taifa lililoketi jijini Dodoma wiki iliyopita
Wakuu wa Idara za Makao makuu UVCCM wakifuatilia mazungumzo ya Katibu Mkuu UVCCM Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) alipokuwa akiwatambulisha kwa watumishi wa UVCCM makao makuu.
Watumishi wa UVCCM makao makuu wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) alipokuwa akiwatambulisha wakuu wa idara za UVCCM  makao makuu kwao
Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Siasa Ndg Peter Kasela akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg.Hassan Bomboko  akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Kamana Juma Simba  akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Uchumi na Uwezeshaji Ndg.Nelson Lusekelo akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) akiwakabidhi Mpangokazi wa Utekelezaji wa UVCCM Mwaka 2018/2019
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) akiwaongoza wakuu wa Idara za Makao makuu ya Umoja wa Vijana wakati akiwatembeza maeneo mbali mbali ya Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam(Picha na FahadiSiraji wa UVCCM)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.