Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Azungumza na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

Na.OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke.
Pamoja na mambo mengine Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alimpa taarifa Makamu wa Rais juu ya ziara ya Mwanamfalme William wa Uingereza, atakayewasili nchini wiki ijayo kwa ziara yake ya siku tatu yenye lengo la kujifunza mambo ya uhifadhi wa wanyamapori 
kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dunia unaohusu masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori utakaofanyika London, Uingereza mwezi Oktoba. Aidha Balozi Cooke alimjulisha Mhe. Makamu wa Rais utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Aprili 2018, jijini London, Uingereza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.