Habari za Punde

Rastazoni Yatinga Hatua ya Pili Michuano ya Kuadhimisha Miaka 61 ya Timu ya Ujamaa Zanzibar Baada ya Kuifunga Timu ya Kundemba Kwa Penenti 3-2 M chezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan leo.

Mchezaji wa Rasta Zoni Ramadhani Issa akiwapita mabeki wa Timu ya Kwendemba wakati wa mchezo wao wa Ufunguzi wa Michuano ya kusherehekea Miaka 61 ya Klabu Kongwe Zanzibar ya Ujamaa, mchezo huo umefanyika katika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Timu hizo zimeonesha mchezo wa ufundi na kila upande ukimtegea mwezake na kuleta mashambulizi ya kupokezana T
Timu ya kKundemba itabidi ijilaumu kutokana na washambuliaji wake kupoteza nafasi nyingi katika lango la Rastazoni. hadi kipindi cha kwanza kinamaliziki timu hizo zimekuwa sare ya bila kufungano.
Kipindi cha pili kiliaza kwa mashambulizi langoni kwa timu ya Kundemba na mshambuliaji wa timu ya Rastazono imekosa goli wakati akijaribu kumpiga chenga kipa wa Kundemba na kuushika mpira huo.
Mchezo huo umeamulia kwa njia ya mikwaju ya penenti Timu ya Kundemba imepata peneti 2 na Timu ya Rastazoni imepata penenti tatu. 
 Mshambuliaji wa Timu ya Rastazoni Cosmas Bukombe akijaribu kumpita Kipa wa Timu ya Kundemba Mahmoud Ali wakati wa mchezo wao wa Kuwania Kombe la Kuadhimisha miaka 61 ya Timu ya Ujamaa tangu kuazishwa kwake katika mwaka 1957.
 Mshambuliaji wa Timu ya Rastazoni Ramadhani Issa akimpita beki wa Timu ya Kundemba Omar Mzee wakati wa mchezo wao wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Ujamaa Kuadhimisha Miaka 61 tangu kuazishwa kwake na kushinda mchezo huo kwa penenti 3-2.
 Mshambyliaji wa Timu ya Rastazoni Bakari Rashid akijaribu kumpita beki wa Timu ya Kundemba Ali Mohammed wakati wa mchezo wao wa Kombe la Ujamaa kutimiza miaka 61, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Rastazoni imeshinda kwa penenti. 3-2. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.