Habari za Punde

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 09.09.2018: Zidane, Terry, Neves, Griezmann, Terry, Howe, Fabregas,

Zinedine Zidane amekuwa akiandaa orodha ya wachezaji ambao atawasainia ikiwa ataulizwa kuchukua mahala pake Jose Mourinho kama meneja wa Manchester United. (Sunday Mirror)
Nahodha wa zamani wa Chelsea na England John Terry, 37, anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Spartak Moscow. (Sky Sports Italy)
Kwingineko Terry atasaini mkataba wa miaka miwili baada ya kupita uchunguzi wa afya nchini Italia. (Observer)
John TerryHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJohn Terry
Terry anatarajiwa kulipwa pauni milioni 1.8 kwa mwaka baada ya ushuru kwenye mji huo mkuu wa Urusi. (Sunday Telegraph)
Manchester United na Manchester City wote wana nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Wolves mreno mwenye miaka 21 Reuben Neves mwezi Januari. (Sun on Sunday)
Meneja wa Bournemouth Eddie Howe atasaini mkataba mpya wa pauni milioni 4 kwa mwaka. (Sunday Mirror)
Eddie HoweHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEddie Howe
Mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye miaka 27 Mfaransa Antoine Griezmann anasema anataka kumalizia taaluma yake huko MLS - kwa LA Galaxy au klabu mpya ya David Beckham Inter Miami. (L'Equipe - in French)
AC Milan wanammezea mate kiungo wa kati wa Chelsea wa miaka 31 Mhispania Cesc Fabregas. (Corriere dello Sport - in Italian)
Aston Villa walikuwa na matumaini ya kumsaini John Terry lakini sasa watamtaka mlinzi wa zamani wa Leicester mjerumani Robert Huth, 34. (Sunday Mirror)
Cesc FabregasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCesc Fabregas
Watford wamekubali kumsaini mshambuliaji mwenye miaka 18 Filip Stuparevic mwezi Januari. (Sportski zurnal - in Serbian)
Yasin Ben El-Mhanni, Wing'a wa zamani wa Newcastle, anatafutwa na vilabu vya Ubelgiji Royal Antwerp na Standard Liege. (Sun on Sunday)
Vilabu vya Uingereza vinatathmini mwezi wa Januari kuwa fursa ya mwisho kusaini wachezaji wachanga wa Ulaya kabla ya Brexit kufanya hali hiyo kuwa ngumu. (Sunday Telegraph)
Beki wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos, 32, alisema kuwa hakutaka kumjeruhi mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26 Mohamed Salah katika fainali ya kombe la vilabu bingwa na fikra zake ziko wazi alichofanya usiku huo. (Telegraph)
Sergio Ramos na Mohamed SalahHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSergio Ramos na Mohamed Salah
Mkufunzi wa Uingereza Gareth Southgate hana haraka ya kutia saini kandarasi mpya licha ya shirikisho la soka nchini humo FA kutaka kumpatia nyongeza muhimu ya mshahara. Mkataba wa Southgate unakamilika 2020. (Times - subscription required)
Southgate anafikiria kumchagua Marcus Rashford kwa mechi ya Jumamosi ya ligi ya kimataifa dhidi ya Uhispania -licha ya mshambuliaji huyo wa Manchester United , 20, kuanzishwa mechi moja pekee na timu yake kufikia sasa. (Mirror)
Beki wa Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen, 31, anatarajiwa kutia saini kandarasi ya mwaka mmoja katika mkataba wake ambao unakaribia kukamilika mwisho wa msimu huu. (Sun)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.