Habari za Punde

Viongozi wa Mabaraza ya Vijana Wilaya ya Kati na Mji Wajengewa Uwezo wa Ubunifu wa Bidhaa Kwa Ujasiriamali Zanzibar.

Muwezeshaji kutoka Jumuiya wa Wanasheria Wawanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud akiwasilisha Mada kuhusiana na Ubunifu wa Bidhaa kwa Vijana wa Mabaraza la Vijana ya Wilaya ya Kati na Mjini Unguja kuweza kujengewa uwezo wa kufanya biashara kujikwamua na Ajira na kujipatia kipato kutokana na kazi zao za Ujasiriamali wa Bidhaa mbalimbali. 
Mafunzo hayo yameandaliwa na ZAFELA kuweza kuwajengea uwezo kujikwamua na ajira. 

Muwesilishaji wa Mada katika mafunzo ya kuwajengea Uwezo Vijana wa Baraza ya Vijana wa Wilaya ya Kati na Mjini Unguja yaliofanyika katika ukumbi wa Umoja wa Walemavu Zanzibar na kuwashirikisha Vijana kutoka Mabaraza la Vijana Unguja.  
Vijana wa Mabaraza la Vijana kutoka Wilaya ya Kati na Mjini wakifuatilia mafunzo hayo ya kuwajengea Uwezo wa kubuni bidhaa kwa ajili ya Ujasiriamali wa vidhaa mbalimbali kuweza kujikwamua na kujiongezea kipato.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.