Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Miji Duniani Yaadhimishwa Katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Mkuu wa Idara ya Tehema Kamisheni ya Ardhi Zanzibar Ndg. Mohammed Zahran akizungumza wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Miji Duniani ilioadhimishwa katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar na kuwashirikisha Wadau mbalimbali wa Miji ya Unguja, Maadhimisho hayo yameandaliwa na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Kamesheni ya Ardhi Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa Siku ya Miji Duniani wakifuatilia Mkutano huo wa kutowa Taarifa ya Miji ya Zanzibar wakati wa hafkla hiyo ya Maadhimisho katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mwakilishi kutoka World Bank Bi. Khadija Abdallah Ali akitowa maelezo kuhusiana na GIS & UAV Pilot ukuaji wa Miji na majengo katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Unguja na Pemba wakati wa Maadhimishi ya Siku ya Miji Duniani ilioadhimishwa katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mtoa Mada Mohammed Kassim akielezea kuhusiana na Cola Sayer and Mapping, akitowa mada wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Miji Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 

Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Miji Duniani wakifuatilia hafla hiyo katika ukumbi wa sheikh Idirsa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.