Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Akifungua Kituo Cha Watu Wenye Ulemavu Cha Jimbo la Shauri Moyo Zanzibar Kilichojengwa na Mradi wa Best of Zanzibar Pennyroyal

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikizindua Rasmi Kituo cha Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo kilichojengwa pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni Mjini Zanzibar.Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakishangilia baada ya kukizindua Kituo cha Watu Wenye Ulemavu Jimbo la Shauri Moyo kilichojengwa na Kampuni ya Pennyroyal Zanzibar, Kwa Ajili ya Wananchi  wa Jimbo hilo uzinduzi huo umefanyika katika Kituo hicho Mikunguni Unguja. 
Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali akiangalia na kufurahia bidhaa zinazozalishwa na Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo ndani ya Kituo kipwa alichokizindua rasmi.
 Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa Kituo cha Watu wenye ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo Bibi Mrashi Mikidadi akiwasilisha Risala kwenye hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi.
Balozi Seif akimkabidhi Baskeli Mtoto mwenyeulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo Feisal Mbarouk kwenye hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi hapo Mikunguni.
Mtoto Lutfia Mohamed ambae ni mlemavu akifurahia Baskeli mpya aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi zilizotolewa na Wafadhili mbali mbali.
Fundi Seremala wa Kituo cha Watu wenye ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo Bwana Juma Abdulaah Juma akipokea Baskeli yake itakayomsaidia katika harakati zake za Kimaisha. Picha na – OMPR –ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.