Habari za Punde

Mafunzo kwa waandishi wa habarikuhusu mafunzo ya uwasilishaji wa mkataba ZURA

Na Mwashungi Tahir      Maelezo        
MAMLAKA  ya Udhibiti wa huduma za  Maji na Nishati ZURA imewataka wananchi kupeleka malalamiko yao kwenye baraza lililoanzishwa  ZURA kwa  lengo la kutatua matatizo yanayowakabili  wateja wao na kuyapatia ufumbuzi  kwa haraka.
Hayo ameyasema Afisa huduma kwa wateja ZURA  Ahlam Saleh Khamis wakati alipokuwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari huko kwenye ukumbi wao uliopo Maisara  akiwasilisha mada mbili ambazo ni uwasilishaji wa mkataba wa Huduma kwa wateja na mafunzo juu ya taratibu  za utatuzi wa malalamiko wa ZURA.
Amesema Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati ni Taasisi iliyoanzishwa kwa ajili ya kusimamia na kudhibiti huduma za maji na nishati  pia ina jukumu ikiwemo kuhakikisha huduma zinazodhibitiwa zinapatikana kwa ubora wa hali ya juu.
Hivyo amesema wanahakikisha wanatoa huduma zilizo nzuri na kiwango kinachokubalika kwa ufanisi pamoja na kuwa na uwezo wa kifedha wa kufanya shughuli zao na kupokea malalamiko ya wateja na migogoro baina ya watoa huduma na wateja wao.
“Zura tunahakikisha tunatoa huduma zilizo bora kwa wateja wetu na kuhakikisha tunawahudumia kwa umakini na kuwataka kulitumia vyema baraza lililoanzishwa kwa lengo la kutatua matatizo yao”, alisema afisa huyo.
Akizungumzia kwa upande wa mkataba huo amesemaZura imetayarisha mkataba na kufunga na wateja wake kwa lengo la kuwahakikishia utoaji wa huduma zilizo bora na umetayarishwa kulingana na muongozo uliotolewa na kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2004 kwa kutoa huduma kwa wateja na taasisi za Serikali.
Amesema Mkataba huo una dira, Dhamira na maadili ya Msingi uwazi na uwajibikaji , uadilifu , kujitegemea,ufanisi na ustadi  na mashirikiano katika kazi na umahiri.
Kwa upande wa mada ya taratibu za utatuzi wa malalamiko kwa ZURA  alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za ZURA mteja mwenye malalamiko juu ya huduma zinazodhibitiwa na ZURA anatakiwa kwanza awasilishe lalamiko kwa mtoa huduma kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Vile vile mteja awasilishe lalamiko hilo kwa barua na kutunza nakala ya barua hiyo hivyo matumaini ya ZURA ni watoa huduma wataboresha ufanisi na mafunzo ya kutatua migogoro ya ndani ili kupunguza idadi ya malalamiko.
Nae Afisa uhusiano ZURA Mbaraka Hassan Haji akitoa ufafanuzi wa kanuni zinazosimamia uendeshaji wa Biashara ya Gesi ya Kupikia  alisema ZURA inahakikisha kuwa usalama na afya za watu pamoja na mali zao vinalindwa na kwamba hakuna athari za kimazingira zinazoweza kutokea wakati wa uendeshaji wa biashara hiyo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.