Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Akitembelea Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Balozi Seif akiwasisitiza Wahandisi kuzingatia usalama wa Wananchi katika harakati zao za Matengenezo ilizisije leta athari yoyote wakati wa matumizi ya Uwanja huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa wakikagua maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Gombani Chake Chake Pemba.
Balozi Seif akisisitiza baadhi ya masuala kukamilishwa ili lengo la kuutumia uwanja huo kwa Sherehe za Maadhimisho ya Kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zifanikiwe.
 Haiba ya Uwanja wa Gombani inavyoonekana kwa mbali ikipendeza na kufurahisha.
Balozi Seif na Wajumbe wa Kamati yake ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa wakikagua Bara bara ya Kilomita Tatu katika eneo la Wawi Mbaoni inayotarajiwa kufunguliwa ndani ya Sherehe za Mapinduzi.
Msimamizi wa Ujenzi wa Bara  bara ya Wawi Mbaoni ya Kilomita Tatu Mhandisi Michael Asungwile akitoa maelezo kwa Balozi Seif  ya hali halisi ya ujenzi wa Bara bara hiyo.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewaagiza Wahandisi wa Matengenezo ya Uwanja wa Michezo wa Gombani Chake chake Pemba kuzingatia usalama wa Wananchi watakaoingia kwenye Uwanja huo kwa ajili ya shughuli au sherehe zozote zile.
Alisema usalama wa Wananchi katika maisha yao ya kila siku na sehemu yoyote ile ni jambo la msingi na la kuzingatiwa na Wahandisi na hata Watumishi wa Umma kuliko kitu chengine chochote.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara fupi ya kuangalia maendeleo ya matengenezo makubwa ya Uwanja wa Michezo wa Gombani Chake Chake Pemba unaotarajiwa kutumika kwa Kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964..
Akiambatana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif  alieleza kuridhika kwake na hatua iliyofikiwa  ya matengenezo hayo inayofanywa na Wahandisi Wazalendo kutoka Wakala wa Ujenzi Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wahandisi hao kuendeleza jitihada zao ili lile lengo la Taifa la kuutumia Uwanja huo kwa maadhimisho ya ya Sherehe hizo Mwaka ujao yafanikiwe vyema.
Akiikagua Bara  bara ya Kilomita Tatu iliyopo katika eneo la Wawi Mbaoni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashauri Wajenzi wa Bara bara hiyo kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili iwahi kuzinduliwa ndani ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Balozi Seif  alisema Bara bara hiyo mbali ya kuwa kiungo kwa wasafiri  wa Anga wanaoingia na kutoka Pemba  lakini pia itapunguza usumbufu wa hudumja za Mawasiliano kwa Wananchi wa Maeneo ya Waawi Mabaoni.
Mapema Msimamizi wa Ujenzi wa Bara bara hiyo kutoka Kampuni ya Mecco Mhandisi Michael Usunguwile alimueleza Balozi Seif  kwamba Wahandisi wa Ujenzi huo wanatarajiwa kuanza kuiwekea Lami kuanzia Alhamisi ya Tarehe  27 Disemba.
Mhandisi Michael alisema Wahandisi hao wana uwezo wa kuweka Lami Mita Mia Tano kwa siku kazi ambayo inaweza kuchukuwa muda wa Siku sita hadi kukamilika kwake.
Michael alielezea matumaini yake kwamba kazi hiyo inatarajiwa kuwahi katika muda uliopangwa endapo hakutakuwa na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoweza kuleta athari ya zoezi hilo muhimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.