Habari za Punde

Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Uweleni Mkoa wa Kusini Pemba.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Uweleni Mkoa wa Kusini Pemba.
 Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Uweleni wakishangiria kumpokea mgeni rasmi wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo lao la Skuli ya Sekondari.
 Haiba ya Jengo Jipya linalojengwa katika Skuli ya Sekondari ya Uweleni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Uweleni wakifuatilia hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli yao inayojengwa ya Ghorofa.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Ustaadhi Khamis Ali wa Wilaya ya Mkoani baada ya kusoma Quran kwenye hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondai ya Uweleni Kusini Pemba.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mheshimiwa Mmanga Mjengo Mjawiri akitoa ufafanuzi wa takwimu za ongezeko la Skuli Nchini kabla na baada ya Mapinduzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akizungumza na Wananchi wa Pemba  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Uweleni Pemba.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.