Habari za Punde

Uchomaji wa Mkaa Unaleta Athari Kubwa Kimazingira Kiuchumi na Kijamii.

Na Masanja Mabula -Pemba..27/02/2019.
ASASI  isiyo  ya Kiserikali ya Misitu ya Jamii Pemba (Community Forests Pemba-(CFP) , imesema suala la uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za uchomaji wa mkaa unaleta athari kubwa kimazingira , kiuchumi na kijamii.
 MKurugenzi  Mtendaji wa Asasi  hiyo Mbarouk Mussa Omar amesema  katika kukabiliana na hali hiyo, wameanzisha   tanuri la kuchomea makaa ambalo ni rafiki  wa mazingira.
Amesema kwamba kwa sasa tanuri hilo ambalo ni la majaribio linasimamia na Wizara ya Kilimo , Maliasili na Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano wa asasi hiyo.
Mbarouk amesema kuwa , Wizara ya Kilimo wanasimamia na baada ya muda watatoa tamko juu ya kuendelea kuenezwa tanuri katika maeneo mengine.
“Tanuri hii ni mkombozi wa mazingira , kwani itasaidia kuyalinda na kuhifadhi kutokana na kwamba inatumia kuni kidogo lakini kipato chake ni kikubwa”alifahamisha.
 Suleiman Juma Khamis   kutoka Idara ya Misitu  na Maliasili zisizorejesheka Pemba , amesema iwapo wananchi  watayatumia tanuri hiyo itapunguza uharibifu wa mazingira na kuilinda ardhi.
Aidha amesema tanuri hiyo inauwezo wa kudhitbi ukataji wa miti ovyo, kwani inatumia kuni kidogo kuliko kutumia tanuri za kizamani ambazo huharibu mazingira.
“ Tanuri hii pia inasaidia kuilinda ardhi kwani wanaoitumia katika tanuri za kawaida mbali na kukata miti ovyo , pia huharibu ardhi ya kilimo”alifahamisha.
Mmoja wa wadau wa mazingira Yahya Khatib Suleiman  na fundi wa ujenzi wa tanuri hiyo Julius Gachiri wamesema taunuri hiyo litasaidia utunzaji wa mazingira.
Yahya amewataka wananchi hususani wachomaji wa mkaa, kuichangua fursa hiyo na kuanza maandaliz ya kujenga tanuri wakati Wizara itakapotoa maamuzi yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.