Habari za Punde

Wanafunzi kutoka China wasema SUZA ni chuo bora zaidi kujifunza kiswahili

 Mwanafunzi wa Lugha ya Kiswahili kutoka Beijing China Hasina akiwasilisha Utafiti  unaohusu Uchoraji wa Tingatinga katika kukamilisha masomo yake ya miezi minne Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kampasi ya Vuga.
 Mwanafunzi Lulu kutoka Mjini Beijing China akiwasilisha Utafiti wa mchango wa Siti Bint Saad katika maendeleo ya Taarab Zanzibar  akiwa katika hatua ya mwisho za kumaliza mafunzo ya miezi minne ya kujifunza lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Kampasi ya Vuga.
 Mwanafunzi Nina kutoka Mjini Beijing China akiwasilisha Utafiti wa Mlingano na tofauti baina ya majengo ya China na majnego ya Zanzibar akiwa katika hatua za mwisho za kumaliza mafunzo ya miezi minne ya kujifunza lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Kampasi ya Vuga
 Mwanafunzi Bahati kutoka Beijing China akiwasilisha Utafiti wake juu ya Utalii ni uti wa mgongo katika maendeleo ya Taifa akiwa katika hatua za mwisho za kumaliza mafunzo ya miezi minne ya kujifunza lugha ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Kampasi ya Vuga
Mkuu wa Idara ya Kiswahili kwa Wageni Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Zainab Ali Iddi akiwapongeza Wanafunzi watano wa China wanaojifunza Kiswahili Chuoni hapo baada ya kuwasilisha tafiti walizofanya katika kukamilisha masomo ya miezi minne katika Kampasi ya Vuga.
Picha na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.