Habari za Punde

Naibu Waziri OMPR azindua mkakati wa miaka mitano wa baraza la taifa la watu wenye ulemavu

Zanzibar.                                        05-04-2019.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Mihayo Juma Nunga amesema kukamilika kwa Mpango Mkakati wa Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu Zanzibar kutaiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake kwa usahihi zaidi ukulinganisha na hapoa mwanzo.
Akifunguwa Mkutano wa Wadau juu ya mpango makakati wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini amesema Mkakati huo utatoa miongozo ya utelelezaji wa majukumu ya Baraza hilo jambo ambalo litapelekea kufanya kazi kwa ufanisi.
Amesema tokea kuanzishwa Baraza hilo mwaka 2008,linafanya kazi bila mpango mkakati jambo ambalo limepelekea kuwepo kwa vikwazo katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.
Aidha ameliagiza Baraza hilo kusimamia majukumu yake ipasavyo ikiwemo kusimamia Sera ya Miondombinu rafiki kwa Watu wenye ulemavu ili iweze kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa Watu hao.
Pia amewaomba Wadau hao kutoa mawazo yatakayosaidia kuimarisha Mkakati huo kwa Faida ya Watu wenye ulemavu na Taifa kwa ujumla hasa ukichukulia kila mtu ni mlemavu matarajiwa.
Hata hivyo amesema Miongozo ya Dini na Sheria za nchi inazokataza  kudhalilishwa Watu wenye Ulemavu hivyo ni vyema kuiheshimu na kuacha kuwadhalilisha Watu hao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar Abeida Abdallah Rashid amesema Serikali inafanya juhudi kubwa katika kushughulikia masuala ya Watu wenye ulemavu na tayari mabadiliko yameweza kuonekana ukilinganisha na mika iliopita.
Aidha amewataka wazazi na walezi kuacha kuwabaguwa watu wenye ulemavu kuhusiana na ulemavu wao na kusahau kuwa kila mtu ni mlemavu matarajiwa.
Hata hivyo amewaomba wadau hao kushirikiana katika kuhakikisha mkakati huo unakamilika haraka na kuweza kusaidia masuala ya watu wenye ulemavu katika meneo yao.
Wakichangia Mkakati huo Wadau hao wameliomba Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu kuangalia zaidi masuala ya Watu wenye ulemavu,Kupata Idadi halisi ya Watu hao na kuandaa mazingira yatakayoweza kusaidia wakati panapotokea Majanga ya Kitaifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.