Habari za Punde

NMB Kuwaunganisha Wafanyabiashara Kisiwani Pemba Kupitia Benki ya NMBMKUU wa Wilaya ya Chake Chake Ndg.Rashid Hadid Rashid, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inaunga mkono juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na bank ya NMB, katika kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kisiwa cha Pemba, jambo linaloweza kupelekea kuongezeka kwa mapato ya nchi.

Alisema wafanyabiashara ni watu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, katika suala zima la kukusanya mapato.

Alisema malengo ya Serikali ya awamu ya saba ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhakikisha, inaboresha mapato ya serikali kupitia kodi na kuziba mianya yote ya ukwepaji wa kodi, ambayo husababisha upotevu wa mapato ya serikali hali inayopelekea kuzoretesha maendeleo ya nchi.

Mkuu huyo wa Wilaya ya aliyaeleza hayo, mjini chake chake wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa Pemba, ikiwa ni klabu ya kwanza kisiwani hapa kuanzishwa na NMB.
“Muunganiko huu pia utaweza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, katika suala la kodi na jinsi ya kutunza fedha, jambo hili ni muhimu litaweza kusaidia malengo ya wafanyabiashra, ili kuweza kujengewea uwelewa katika suala zima la ulipaji wa kodi”alisema.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema, kuanzishwa kwa klabu hiyo itaweza kutoa mwangaza kwa wafanyabiashara, kupata mafunzo mbali mbali ya biashra, pamoja na kuelimishwa juu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara, masoko, huduma nzuri kwa wateja, upangaji wa bei, sheria za biashara na mahesabu ya fedha.

Akizungumzi juu ya suala la riba, mkuu huyo wa Wilaya amezitaka taasisi za kifedha Kisiwani Pemba, kupunguza riba katika mikopo yao wanayoitoa kwa wajasiriamali wanaofika kuomba mikopo hiyo.

Alisema baadhi ya taasisi za kifedha, zimekua ni mzigo kwa wajasiriamali masikini, baada ya kupata mikopo hiyo na kushindwa kuirudisha kwa wakati, hali inayopelekea kupoteza mali zao ambazo wameziwekea dhamana ikiwemo nyumba za kuishi.

“Nivizuri kwa makampuni sasa kuangalia utoaji wa bidhaa taslimu, wakati wa ukopaji kwa wafanyabiashara na sio kwa kutoa fedha”alisema.

Aidha aliwataka wafanyabiashara kufanya utafiti kwa kina wa biashara wanayotaka kuifanya, kabla ya kuomba mkopo ili fedha wanazopatiwa waweze kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, pamoja na benk kufuatilia wafanyabiashara waliowapatia mikopo na kujuwa biashara zao ipasavyo.

Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salam Badru Iddi, alisema NMB imeamua kuwafikia wananchi wote wa kipato cha chini Tanzania nzima, kwani mwaka 2018 walifungua klabu za wafanyabiashara 50 Tanzania na mwaka 2019 mikakati yao ni kufungua klabu 36 Tanzania ikiwemo ya Kisiwani Pemba.

“Kuwepo kwa Klabu hizi ni kuwaweka pamoja wafanyabiashara wa Pemba, kuwa na sauti moja katika kuwasilisha au kutetea mambo yao palewanapota matatizo”alisema.
Akizungumzia suala la riba, alisema hicho ni kilio cha muda mferu kwa wateja wa Zanzibar, tayari wameshaliwasilisha katika bodi, ili kusubiri Baraka na kuanzishwa kwa benk ya kiislamu.

Meneja wa NMB Tawi la Pemba Ahmed Nassor, alisema amefarajika sana kwa Pemba, kuanzishwa kwa klabu ya wafanyabiashara, kitu ambacho kitaweza kuwaweka pamoja wafanyabiashara wa Pemba.

Mtaalamu wa mafunzo kutoka EIB Erick Chrispin, aliwataka wafanyabiashara kutambua umuhimu wa nidhamu ya fedha, kwani ni rahisi kujua kinachoingia na kinachotoka katika biashara zake.

Hata hivyo aliwataka wafanyabiashara kuweka kumbukumbu za mauzo, manunuzi na gharama wanazotumia katika biashara zao, kwani kufanya hivyo kutamuwezesha mfanyabiashara huyo kuwa na nidhamu ya fedha zake.

Wakitoa ushuhuda wao mashuhuda ambao ni wafanyabiashara na wateja wa NMB, wameita benk hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, pamoja na kuwa msari wa mbele katika kusaidia jamii huda mbali mbali.

Katika mkutano huo wafanyabiashara wameweza kumchagua Abdalla Ali Said (Ngonda) kuwa mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara Pemba, huku nafasi ya katibu wa klabu hiyo ikimuangukia Rabia Said Omar, sambamba na wafanyabiashara 10 kupatiwa vyeti maalumu na NMB.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.