Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma Azungumza na Watendaji wa Wizara




 It





WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma amewataka watendaji wa Wizara hiyo kutunza Siri za Wizara Kama walivyoahidi katika viapo vyao vya kazi.

Akizungumza na watendaji wote wa Wizara yake katika Skuli ya Sekondari  Haile sselassie  amesema ni kosa la jinai kwa mtumishi wa Serikali kutoa Siri na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mtumishi atakae kwenda kinyume na agizo hilo.

Amesema kila mtumishi anapokuwa katika uajiri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ajue anafata ilani ya Chama Cha  Mapinduzi, hivyo amewataka kutumia itikadi zao wanapokuwa nje ya Ofisi na baada ya kumaliza majukumu yake aliopangiwa.

Aidha Mhe Riziki amewataka wakurugenzi, Wakuu wa divisheni na vitengo vilivyomo katika Wizara ya Elimu kuweka utaratibu wa kuwapongeza watendaji waliochini yao pale wanapofanya vizuri katika majukumu yao ili kuwatia ari ya kuzidi kuipenda kazi yao.

Nae Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said amewasisitiza watumishi wa Wizara yake kuwa na mashirikiano katika kazi kwani huleta hamasa ya utendaji mzuri wa kazi pamoja na kuondosha ubinafsi ambao unaweza kukwamisha  maendeleo katika sekta ya Elimu nchini.

Nao wafanyakazi wa Wizara hiyo wameiomba Wizara ya Elimu kuzungumza na wahusika wa Halmashauri juu ya kutambua wajibu wao wa kazi kwani kumeonekana kuwepo na mvutano kati ya wafanyakazi wa Wizara na Halmashauri hasa katika masuala ya ugatuzi.

Hata hivyo wameiomba Wizara kutoa sauti yake juu ya masuala ya udhalilishaji kwani baadhi ya wahusika wengi wa kesi hizo ni walimu ambao wanasababisha kuishusha hadhi fani hiyo na kusaidia kutokomeza kabisa vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.