Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Yakabidhi Msaada wa Vyakula Kwa Vituo Vya Watoto Yatima na Wazee Zanzibar.

Afisa wa Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limite. Mohammed Khamis Ismal, akikabidhi msaada wa Vyakula kwa Mlezi wa Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar, ikiwa ni kawaida kwa PBZ kutowa Msaada kwa Vituo Vya Watoto Yatima na Wazee, kwa ajili ya futari.   


Na. Muhammed Khamis

Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ)  imesema itaendelea kuwajali na kuwahurumia watoto na wazee wenye mahitaji maalumu kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa wateja wao.
Hayo yamesemwa na Afisa masoko wa benki hio Muhammed Khamis Ismail wakati alipokua akikabidhi msaada wa chakula aina mbali mbali katika nyumba za watoto yatima Mazizini pamoja na kituo cha kulele watoto cha SOS.
Alisema kuwa kikawaida hufanya hivyo kila ifikapo mwezi wa Ramadhani kwa lengo la kuwaonesha kuwajali na kuwafariji watoto hao na wazee kama sehemu ya jamii yenye mahitaji maalumu.
Alieleza kuwa utaratibu huo ni wazi kuwa hufawanya wahusika kujihisi ni miongoni mwa jamii na kwamba jumla ya vituo kumi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba wamefaidika na msaada huo.
Akitaja baadhi ya vitu hivyo ni alisema ni sukari,mchele mafuta ya kupikia pamoja na unga ambapo gharama yake ni milioni thalathini na saba.
Hata hivyo Ismail alisema anaamini kuwa msaada huo kwa wahusika utakwenda kuondoa ugumu wa maisha hususani katika kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Awali akipokea msaada huo mwakilishi wa kituo cha kulelea watoto wa kituo  cha SOS Maida Mussa alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka ambapo watoto wao wana mahitaji.
Alisema kitendo kinachofanya na benki ya watu wa Zanzibar ni chakupigiwa mfano na niwazi inaonesha ni yenye kujali jamii ya watu wa chini.
Mmoja miongoni mwa watoto wanaoishi katika nyumba hizo alisema msaada huo utawafanya wajihisi ni miongoni mwa watoto wenye kuishi katika jamii z akawaida na kutojisikia wanyonge katika kipindi hichi cha mwezi wa Ramadhan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.