Habari za Punde

DC KASESELA: MARUFUKU KUFANYA BIASHARA IRINGA KAMA HULIPI KODI AU HUNA KITAMBULISHO CHA MACHINGA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizunguza na wafanyabiashara wa bidha za kusindika walikuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali
Wafanyabiashara wa bidha za kusindika wakiwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali na wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa bidhaa za kusindika

Na.Fredy Mgunda -Iringa.
Wafanyabiashara wa wilaya ya Iringa wametakiwa kufanya biashara wakiwa wamelipa kodi au wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama kitambulisho cha machinga.

Akizungumza na wajasiliamali waliokuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema ni marufuku kwa sasa kufanya biashara yoyote wilaya ya Iringa bila kulipa kodi na zile ambazo hazijafikia hatua kodi zitalipa tozo

“Sasa tunaanza kufanya mchakato wa kuchunguza kujua wafanyabiashara wangapi wanafanya kazi hizo bila kulipa kodi na tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyosema” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wafanyabiashara wadogowadogo wote wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanapata kitambulisho cha kwa shilling elfu ishirini ambacho kinatamruhusu kufanya biashara sehemu yoyote hapa nchini kwa mujibu wa Rais

“Jamani ili ufanye biashara kwa uhuru katika wilaya ya Iringa ni lazima uwe na kitambusho cha wafanyabisahara wadogo au uwe umelipia leseni kutoka katika mamlaka husika la sivyo huwezi kufanya biashara hiyo wilaya ya Iringa” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wananchi wote wanaopenda kufanya biashara kuhakikisha wanafanyabiashara kwa kufuata taratibu zilizowekwa na nchi ili wasipate usumbufu wowote ule kutoka kwa mamlaka za wilaya ya Iringa.

“Jamani wananchi wa Iringa changamkieni kuchukua vitambulisho vya wafanyabishara wadogo wadogo ili kufanya biashara zenu mkiwa na uhuru wa kutosha ila mkikahidi mkono wa sheria utawahusu” alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwashauri wafanyabishara ya bidhaa za kusindika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata kanuni za kisheria kwa kuhakikisha wanalipa kodi kama inavyostahili.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo walimuadi mkuu wa wilaya hiyo kuwa watahamasishana kuhakikisha wote wanakuwa na vitambulisho hivyo ili wafanye biashara kwa uhuru na haki.

“Mkuu tunakuhakikishia kuwa tutafanyabiashara huku tukiwa tumevaa vitambulisho hivi kwa kuwa Rais wetu katupa uhuru wa kufanya biashara zetu mahali popote pale bora mradi tuwe na vitambulisho hivyo” walisema wafanyabiashara hao

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.