Habari za Punde

Shirika la Afya la Amref lazindua mradi wa Afya Kamilifu Zanzibar Utakaotekelezwa Kwa Miaka Mitano.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Bi.Florence Temu, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Afya Kamilifu Zanzibar  , hafla hiyo imefanyika katika  ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa Afya Kamilifu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli Verde Mtoni Zanzibar.


Na. Haji Mohd
Shirika la Amref Health Afrika limezindua mradi mpya inayolenga  kupanua juhudi za utoaji wa huduma za matunzo na matibabu ya kufubaza VVU visiwani Zanzibar ili kumaliza janga la ukimwi ifikapo 2030.

Mradi huo unaoitwa “Afya kamilifu” unaofadhiliwa na Mpango wa dharura wa Rais wa marekani wa msaada wa kupambana na ukimwi utatekelezwa kwa miaka mitano ambapo umelenga kupanua tiba ya kufubaza virusi ili kutokomeza ugonjwa wa ukimwi. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo Florence Temu katika mkutano wa ufunguzi wa mradi huo huko katika hotel ya Verde Mtoni amesema malengo ya mradi watu walipata maambukizo  waweze kujitambua na  kuweza kupatiwa tiba kwa wakati  ili kufubaza kabisa virusi mwilini. 

Kwaupande wake  Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Afya  Asha Abdalla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar  itaendelea kuunga mkono jitihada za Shirika hilo lenye lengo la kupambana na ugonjwa wa ukimwi Zanzibar. 

Amesema hayo wakati akizindua mradi wa afya kamilifu utaotekelezwa kwa miaka mitano Zanzibar ambao utasaidia kupunguza ongezeko la VVU  na kufubaza kabisa virusi. 

Hata hivyo ameliomba shirika hilo kuongeza nguvu zaidi katika makundi maalum kwani bado maambukizo ni makubwa ukilinganisha na watu wa kawaidia na hii inatokana na vijana kujikita kwenye dawa za kulevya, kufanya mapenzi kwa jinsia  moja  hivyo mashirikiano bado yanahitajika zaidi. 

Aidha amesema Zanzibar  inaasilimia 1 cha kiwango cha maambukizi na hii inatokana na juhudi zinazochukuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kupambana na ungojwa huo. 

Asha ametoa rai kwa shirika hilo pia katika kutekeleza mradi huo hapa Zanzibar   ziwezeshwe serikali za mitaa ili nazo zishiriki katika kutoa elimu katika ngazi za shehia ili wananchi  waweze kujilinda. 

Mapema akitoa ufafanuzi Meneja wa Mradi Edwin Kilimba amesema kwa zaidi ya miaka 30 shirika la Amref Health Afrika limekuwa likishirikiana na serikali ya Tanzania  na wadau wengine kuimarisha mifumo ya afya nchini ili kuondoa changamoto zinazochochea kurudisha nyuma maendeleo. 

Edwin amesema mradi pia utaimarisha ufuatiliaji na tathmini kiasi cha kupata taarifa halisi za maendeleo pamoja na kusaidia mifumo ya usimamizi wa data katika ngazi ya kituo na kujenga uwezo wa umiliki wa data ili kuongeza ubora wa huduma kupitia timu za mkoa za usimamizi wa afya na timu za halmashauri. 

Mradi wa afya kamilifu ni mradi wa miaka mitano unaotekelezwa mkoa wa tanga na visiwani Zanzibar kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali ya TCDC na UMB ambapo mradi huo umefadhiliwa na shirika la marekani la kuzuia na kudhibiti magonjwa CDC. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.