Habari za Punde

LIGI Daraja la tatu wilaya ya Mjini hatua ya.sita Bora inatarajiwa kuanza leo mjini hapa.

Na,Mwanajuma Juma.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo inaonesha kwamba mechi zote za ligi hiyi zitachezwa kwenye uwanja wa Amaan .

Timu zilizoingia hatua hiyo ambazo zimepangwa katika Makunduchi mawili ni 
Kwerekwe Boys, Baja na Polling land zipo kundi A na kundi B ni Maruhubi, Makadara na FC Porto.

Ratiba inanesha kuwa leo kutakuwa na mchezo wa kundi A Kati ya timu ya Kwerekwe Boys na Baja, ambao utachezwa wakati wa saa 10:00 jioni.

Aidha ratiba hiyo inaonesha kwamba kesho uwanjani hapo majira ya saa 10:00 za jioni Maruhubi watashuka Kupambana na Makadara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.