Habari za Punde

Mawakala wa mitandao ya simu wanaofanya kazi kinyume na sheria wawindwa na TCRA

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA  Zanzibar Bi. Esuvatie Masinga akichukuwa maelezo kwa mmoja wa Mawakala wa Usajili wa Simu na Tigo Pesa katika eneo la Darajani Zanzibar wakati wa zoezi la kubaini Mawakala walikuwa hawajasajiliwa na Makampuni ya Simu na kutokuwa na vibali vya makampuni hayo.

Na. Hawa Ally, Zanzibar
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania TCRA ofisi ya Zanzibar kwa kushirikiana na jeshi la polisi imeendesha zoezi la kuwakagua na kuwakamata mawakala wa mitandao ya simu za mkononi wanaoendesha shughuli hizo kinyume cha sheria za TCRA. 

Zoezi hizo ambalo limefanyika eneo la darajani hapa Unguja huku Jumla ya mawakala zaidi ya 50 wamekamatwa kuendelea shughuli zao kinyume cha sheria. 

Akizungumzia zoezi hilo kwa ujumla Mkuu wa TCRA Ofisi ya Zanzibar Esuvatie Masinga amesema lengo la zoezi hilo  ni kufanya ukaguzi na kuwakagua mawakala na freelancer wanaosajili laini  kwa kufata sheria za TCRA. 

Alisema mawakala wengi na freelancer hawana vibali ikiwemo leseni, barua ya idhini kutoka mitandao husika, tin namba pamoja na ofisi jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mamlaka ya mawasiliano.

"utakuta mawakala hawana ofisi maalum badala yake wapo chini ya miamuvuli, hawana hata barua za vibali kutoka mitandao husika ambayo wanaosajili hizo laini hili ni Kosa wa mujibu wa sheria." Alisema 

Hata hivyo ametoa onyo kwa mawakala wanaosajili laini kwa alama ya vidole kuacha kuwatoza wananchi pesa kwani zoezi hilo ni bure

Nae Mhandisi wa TCRA Ofisi ya Zanzibar Mtende Shirazi Hassan amesema mawakala wengi katika zoezi hilo wamekutwa na vitambulisho vya kampuniya simu badala ya barua ya idhini kutoka kila kampuni anazosajili laini hizo . 

Alisema mawakala wengi wanafanya kazi bila ya kuwa na leseni, ofisi inayowataka kuendesha shughuli hizo kisheria. 

Hata hivyo amesema agizo la ukaguzi huo kwa freelancer na mawakala limefanyika kwa utulivu licha baadhi ya wasajili laini na mawakala kufunga vibanda vyao na kulikimbia zoezi hilo. 

Nao makawala hao amewashauri TCRA kutoa taarifa mapema juu ya mabadiliko yoyote yanayotokea Ili waweze kufata sheria na kuepuka usumbufu. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.