Habari za Punde

Mkutano wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharib Ndugu Mohamed Rajab Soud,akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Mkoa huo Mwera Unguja. 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi,Ndugu Zainab Ali Maulid (kushoto),akifungua Mkutano wa Baraza hilo la UWT Mkoa wa Magharibi.
WAJUMBE wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi wakisikiliza nasaha za Mgeni rasmi katika Kikao hicho.
BAADHI ya Wabunge na Wawakilishi wa UWT walioudhuria katika Mkutano wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi.
MJUMBE wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Welezo Dkt.Saada Mkuya, akitoa shukrani kwa niaba ya UWT katika Mkutano huo.

Na.Is-haka Omar -Zanzibar.
JUMUIYA za Chama Cha Mapinduzi Nchini zimetakiwa kuzidisha juhudi katika kufanya kazi za kuimarisha CCM ili Taasisi hiyo iendelee kuwa bora kisiasa Nchini.  

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi Ndugu Mohamed Rajab Soud,wakati akiwahutubia Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la UWT Mkoa wa Magharibi Unguja. 

Amesema Jumuiya za CCM licha ya kufanya vyema katika majukumu yake ya kila siku bado zinatakiwa kuongeza kasi ya kiutendaji na kiubunifu hili kuhakikisha Chama ndani ya Mkoa huo kinaimarika Kisiasa,Kiitikadi na Kiuongozi.

Kupitia Mkutano huo Mwenyekiti huyo Ndugu Rajab, amewambia Akina Mama hao kuwa  Wanategemewa na Chama Cha Mapinduzi katika harakati mbali mbali za Kisiasa hivyo wanatakiwa kutumia uwezo wao wa Kisisa na Kitaaluma ili kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi wa mwaka 2020.

Amesema Akina Mama hao kwa juhudi zao za kutekeleza kwa wakati mwafaka hasa katika kufanya vikao mbali mbali vilivyoelekezwa na Katiba ya Jumuiya hiyo.

Amesema Viongozi na Wanachama kila mmoja kwa nafasi yake wanatakiwa wanatakiwa kuwaeleza Wananchi katika maeneo yao Utekelezaji wa Ilani ya CCM unaotekelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wabunge,Wawakilishi na Madiwani.

Aidha amesema Mkoa huo upo katika maandalizi ya kutekeleza kwa Vitendo kampeni ya Magharibi ya Kijani kwa kuhakikisha Mkoa huo unakuwa ni Ngome imara ya CCM Kisiasa.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo,Ndugu Zainab Ali Maulid amesema Jumuiya hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza kazi mbali mbali za kuleta maendeleo endelevu ndani ya CCM.

Ameeleza kuwa  kwa sasa jumuiya hiyo inaendelea na mipango ya kuongeza Wanachama wapya hasa Wanawake ili kuhakikicha CCM inaingia katika Uchaguzi Mkuu Ujao ikiwa na Takwimu sahihi za Wanachama wenye sifa za kupiga kura.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Jumuiya hiyo,Mbunge wa Jimbo la Welezo Dkt.Saada Mkuya amesema nasaha zilizotolewa na Mgeni rasmi watazifanyia kazi kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.