Habari za Punde

"TUNA OFISI 29 MIKOA YOTE TANZANIA BARA NA ZANZIBAR, FIKENI MUHUDUMIWE": PSSSF

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mkoa wa Temeke, Bi.Ritha Ngalo (kulia) na Afisa Mafao Mfuko wa Mfuko huo, Bw. Salvatory Matemu, wakiwahudumia wanachama wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 10, 2019.

Na. K-VIS BLOG/Khalfan Said
WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) popote pale walipo Tanzania bara na Visiwani, wamesogezewa huduma karibu ambapo Mfuko una jumla ya ofisi 29 mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.
Meneja wa Mfuko huo Mkoa wa Temeke, Bi. Ritha Ngalo, amewaambia waandishi wa habari kwenye banda la PSSSF namba 13 kwenye viwanja vya Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 10, 2019 kuwa kwa wale watakaofanikiwa kufika kwenye Maonesho hayo, yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, wasisite kupita kwenye banda hilo ili wapatiwe huduma sawa na zile wanazohitaji kuzipata kwenye ofisi mbalimbali za Mfuko.
Serikali kupitia Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 2018 ilifuta mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF, PSPF, LAPF  na GEPF na kuanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Waatumishi wa Umma PSSSF.
Maonesho hayo yanatarjiwa kufikia kilele Julai 13, 2019.
Mstaafu Francis Ramadhan Njau, (kulia), ambaye alikuwa Afisa Ushirika Daraja la I, akihudumiwa na Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mkoa wa Temeke, Bi.Ritha Ngalo kwenye banda la Mfuko kwenye viwanja vya Maonesho Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 10, 2019. Aliyesimama kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
Wanachama wa PSSSF, wakiwa tayari wamehudumiwa.
Mwanachama akipatiwa taarifa alizohitaji kutoka PSSSF alipotembelea banda la Mfuko huo Julai 10, 2019.
Afisa Michango PSSSF Bi. Getrude Athanas (kulia), akimpatia maelezo ya kina mwanachama huyu aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald P. Maeda (kulia), akihakikisha kila swali alilokuwa nalo Mwanachama huyu linapatiwa majibu kwa vielelezo.
Meneja wa Mfuko huo Mkoa wa Temeke, Bi. Ritha Ngalo, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Mfuko huo Julai 10, 2019. Kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfukmo huo Bw. Abdul Njaidi.
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mkoa wa Temeke, Bi.Ritha Ngalo (kulia) na Afisa Mafao Mfuko wa Mfuko huo, Bw. Salvatory Matemu, wakiwahudumia wanachama wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 10, 2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.