Habari za Punde

Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) Wapiga Marufuku Choklet na Juisi Fruit Zilizomo wenye Vifungashio Aina ya Bomba la Shindano.

l
Mkurugenzi Idara yaUdhibiti Usalama wa Chakula (ZFDA) Dr. Khamis Ali Omar akitoa taarifa kwa wandishi wa habari ya marufuku ya uzaji wa choklet na frut juisi zilizomo kwenye kifungashio kinachoonekana kama bomba la shindano.
Mkurugenzi Idara yaUdhibiti Usalama wa Chakula (ZFDA) Dr. Khamis Ali Omar akitoa taarifa kwa wandishi wa habari ya marufuku ya uzaji wa choklet na frut juisi zilizomo kwenye kifungashio kinachoonekana kama bomba la shindano.
Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula Idara ya Udhibiti Usalama wa Chakula Mohamed Shadhili Shauri akielezea jitihada wanazochukuwa kuhakikisha bidhaa hiyo inatoka sokoni.
Muandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza swali katika Mkutano huo.
Picha na Makame Mshenga.
Na Faki Mjaka, Maelezo Zanzibar.
Wazazi na Walezi nchini wametakiwa kuepuka kuwanunulia Watoto wao bidhaa aina ya Choklet zilizotengenezwa mfano wa Bomba ya Sindano kutokana na kuingizwa nchi kimagendo bila kuthibitishwa ubora na usalama wake kwa watumiaji.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Usalama wa Chakula (ZFDA) Dr. Khamis Ali Omar wakati akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar kuhusu uwepo wa bidhaa hiyo katika Soko.
Amesema Muingizaji wa Bidhaa hizo hakupita katika Ofisi yake hivyo bidhaa hizo bado hajizasajiliwa wala kupita katika Maabara yao kujulikana ubora na usalama wake.
Aidha Dk. Khamis ameongeza kuwa ZFDA kwa kushirkiana na vyombo vingine vya uchunguzi wanaendelea kumtafuta Mfanyabishara aliyeziingiza bidhaa hizo nchini kinyume na sheria na akipatikana atapelekwa katika vyombo vya Sheria.
“Jukumu la ZFDA kwa sasa ni kuziondoa katika Soko kutokana na kutokidhi vigezo wakati huo huo kwa kushirikiana na vyombo vingine tunamtafuta Mfanyabiashara huyo ili tumpeleke katika vyombo vya kisheria”
Kwa upande wake mkuu wa Kitengo cha usajili wa bidhaa kutoka ZFDA Khadija Ali Sheha amesema bidhaa hiyo siyo halisi kwa vile haioneshi hata Kampuni au Kiwanda kilichotumika kutengeneza bidhaa hiyo.
Amesema katika Vifungashio vya Bidhaa hiyo imeandikwa inatoka nchini China lakini hakuna maelezo ya ziada kuelezea Kiwanda kilichotumika na Jimbo husika nchini China ili kufuatilia zaidi.
Kuhusu kifungashio chake amesema bidhaa hiyo inamlaghai mtoto na hivyo zinaweza kupelekea athari kubwa kwa watoto siku za mbele.
“Kifungashio kinamlaghai mtoto lakini kinaweza pia kuwapelekea Watoto waweze hata kutumia Mabomba ya Sindano ya kawaida kutia maji au juisi wakaanza kutumia na mwisho kupata maambukizi mbalimbali” Alisema Khadija.
Kutokana na hali hiyo tayari Wakala unaendelea na zoezi la kuzichuguza bidhaa hizo katika maeneo tofauti ili zisiwepo katika Soko.
Mohamed Shadhil Shauri Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula ZFDA amesema tayari wamekagua maduka 25 ya mjini na zoezi litaendelea maeneo mbali mbali ya mijini na Vijijini.
Amesema kuna uwezekano wa bidhaa hizo kupitia katika Bandari bubu au kupitia katika Vituo vya forodha bila kufahamika vyema hasa kwa wale Wafanyabiashara wanaochanganya bidhaa tofauti katika Kontena moja.
Jumla ya Maboksi 24 yenye Choklet zipatazo 600 tayari yamekamatwa katika Maduka mbali mbali ili kuondolewa katika Soko.
Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) umeanzishwa chini ya sheria No.2 ya mwaka 2006 na marekebisho yake ya no. 3 ya mwaka 2017 ambapo jukumu lake ni kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa katika soko zipo katika hali ya ubora na usalama kwa ajili ya matumizi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.