Habari za Punde

Wanamichezo Kisiwani Pemba Washiriki Katika Bonaza la Kufunga Mwaka 2019 /2020 Katika Uwanja wa Gombani.

WACHEZAJI wa Timu ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Pemba, katika uvutaji wa kamba wakijitahidi kuwavuta Wizara ya Fedha lakini bahati haikuwa yao na kujikuta wanafunzwa, wakati wa bonanza la kufunga mwaka a fedha 2018/2019 na kufungua mwaka mpya wa fedha 2019/2020
WACHEZAJI wa Timu ya Wizara ya Fedha na Mipango Pemba, wakiwavuta wenzao wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, huku wakitapa mashabiki kutoka kwa wafanyakazi wa Wizara ya Vijana, wakati wa bonanza maalumu la kufunga mwaka wa hesabu 2018/2019 na kufungua mwaka mpya 2019/2020
WACHEZAJI  wa Timu ya Wizara ya Fedha katika Uvutaji wa Kamba, wakishangilia ushindi wao baada ya kuwavuta wenza wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Pemba
WAFANYAKAZI wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, wakimpongeza mfanyakazi mwenzao Najma Abdalla mwenye kuuku baada ya kushinda katika mchezo wafukuzaji wa kuku, wakati wa   bonanza la kufunga mwaka a fedha 2018/2019 na kufungua mwaka mpya wa fedha 2019/2020
NAIBU waziri Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Shadiya Mohamed Suleiman, akisalimiana na wachezaji waTimu ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Pemba,  bonanza la kufunga mwaka a fedha 2018/2019 na kufungua mwaka mpya wa fedha 2019/2020, katika mchezo wafainali na CAG kuibua kwa penat 4-2 dhidi ya Wizara ya Vijana
NAIBU waziri Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Shadiya Mohamed Suleiman, akimkabidhi zawadi ya fedha kwenye boksi na mipita mitatu mshindi wa kwanza wa bonanza la kufunga mwaka a fedha 2018/2019 na kufungua mwaka mpya wa fedha 2019/2020,  katika mchezo wafainali na CAG kuibua kwa penat 4-2 dhidi ya Wizara ya Vijana,  kushoto ni afisa mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba  Ibrahim Salehe Juma. (PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.