Habari za Punde

Meli Mpya ya Mafuta Kuwasili Zanzibar Rasmin Kesho Bandari ya Zanzibar.

Meli Mpya ya Mafuta ilionunuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar MT.UKOMBOZI 2 Kuwasili Zanzibar kesho katika Bandari ya Zanzibar na kukabidhiwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 


HATIMAE ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyowaahidi wananachi wa Zanzibar kuwa Serikali anayoiongoza itanunua meli mpya ya mafuta MV MKOMBOZI II leo imetimia baada ya meli hiyo kuwasili katika pwani ya Zanzibar ikitokea Shanghai nchini China.

Meli hiyo iliyotengenezwa na Kampuni ya DAMEN TANKER ya Uholanzi itawasili rasmi katika Bandari ya Malindi Zanzibar majira ya asubuhi mapema hapo kesho.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliani Zanzibar Ndg Mustafa Aboud Jumbe akizungumza huko Ofisi kwake Kisauni, alithibitisha ujio wa meli hiyo na kueleza jinsi hatua mbali mbali zilizochukuliwa katika mchakato wa kununuliwa kwa meli hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi kuwasili kwake hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.