Habari za Punde

Mkutano wa Kuhusu Takwimu za Makosa ya Barabarani Zanzibar.

 
CPL kutoka kitengo cha Traffic Makao Makuu ya Polisi Zanzibar akijibu maswali ya Waandishi kuhusu makosa  ya  Ajali za Barabarani ambapo ameonekana kushuka kutoka ajali 39 kwa mwezi wa Agosti 2018 hadi 23  Mwezi wa  Agosti 2019 Mkutano uliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir     Maelezo     16-9-2019.
Jumla ya makosa ya barabarani 1,645 ya ukiukwaji wa sheria za barabarani yameripotiwa  katika vituo mbali mbali vya Polisi  mwezi wa Agosti ,2019.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  Afisa wa Kitengo chaTakwimu za ajali  na makosa ya barabarani kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Asha Mussa Mahfoudh  amesema makosa hayo yamepungua kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mwezi wa Julai mwaka huu ambapo yalikuwa 1,749.
Amesema miongoni mwa makosa hayo  ni pamoja na kuzidisha idadi ya abiria , kuendesha gari kwa mwendo wa kasi , kutokuwa na leseni, na kutovaa sare na beji kwa matingo na dereva wa gari za abiria ambapo Wilaya ya Mjini na Magharibi B zinaongoza na kuwa na makosa mengi.
"Miongoni mwa ajali zinasababishwa na wanaoendesha  gari kwa mwendo wa kasi bila kuzingatia sheria za barabarani", alisema Afisa Asha.
Akizungumzia kuhusu ajali za barabarani amesema jumla ya ajali 23 zimeripitiwa kutokea kwa mwezi wa Agosti mwaka huu ambapo waliofariki  ni 14 na waliojeruhiwa ni 22.
Nae Afisa kitengo cha usalama barabarani kutoka Makao Makuu ya jeshi la Polisi Koplo Ali Abdullah Juma amesema  wanaandaa mikakati ya kupunguza ajali barabarani kwa kutoa elimu kwa wananchi kupitia katika sehemu za maskulini na vyuo na kufanya doria kila sehemu mara kwa mara ili kuweza kuchukua hatua za kisheria kwa wale wanaovunja sheria.
Pia tunafanya uperesheni  kwa kushirikiana na baadhi ya vikosi vyengine ili kudhibiti ajali na baadhi ya makosa ya barabarani na kuhakikisha wananchi wanakuwa katikam hali ya usalama.
Sambamba na hayo Mkaguzi wa kitengo cha Takwimu za uhalifu Khamis Mwinyi Bakari alisema wanajitahidi kutoa elimu kwa kupitia kwenye vyombo vya habari hasa wanaotembea kwa miguu na wanaoendesha baskeli ili  wawe waangalifu katika safari zao.
Mtakwimu wa Kitengo cha Takwimu za makosa ya Jinai,Madai na Jinsia Asha Mussa Mahfoudh akitoa Takwimu za Makosa ya  Ajali za Barabarani ambapo ameonekana kushuka kutoka ajali 39 kwa mwezi wa Agosti 2018 hadi 23  Mwezi wa  Agosti 2019 Mkutano uliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano kuhusu Takwimu za Makosa ya  Ajali za Barabarani ambapo ameonekana kushuka kutoka ajali 39 kwa mwezi wa Agosti 2018 hadi 23  Mwezi wa  Agosti 2019 Mkutano uliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Zenj Fm Amina Diwani akiuliza maswali katika Mkutano wa Waandishi  kuhusu Takwimu za Makosa ya  Ajali za Barabarani ambapo ameonekana kushuka kutoka ajali 39 kwa mwezi wa Agosti 2018 hadi 23  Mwezi wa  Agosti 2019 Mkutano uliofanyika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini Zanzibar.

Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.