Habari za Punde

Ziara ya Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Wakiwa Ziarani Kisiwani Pemba leo.

Raia mwema kutoka  Shehia ya Ngwachani Wilaya ya Mkoani Pemba, akiueleza Ujumbe wa Baraza la Mapinduzi unaofanya kazi ya kutafuta mashamba ya Serikali ya eka tatu (3) ambazo zina milikiwa na Wananchi kinyume na utaratibu wa kisheria huko katika eneo la Ngomeni Pemba.
Waziri asiekuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi ,Juma Ali Khatib, akimueleza jambo  mwananchi anaeisaidia Serikali kufichuwa mashamba ya Serikali eka 3 yanayomilikiwa visivyo halali kisheria.
Miongoni mwa mashamba ya Serikali eka 3 zinazomilikiwa na Wananchi binafsi kinyume na utaratibu wa kisheria ikiwa hizo ni miongoni mwa eka 9 zilizoko katika eneo la Ngomeni Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Rashid Hadidi Rashid, akieleza jambo kwa ujumbe wa Baraza la Mapinduzi uliofika katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kuangalia mashamba ya Serikali yanayomilikiwa na Wananchi kinyume na utaratibu uliowekwa huko katika eneo la Ngomeni Chake Chake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.