Habari za Punde

Balozi Seif ziarani Mkoa wa Kusini Unguja kukagua miradi ya maendeleo

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha Unguja Ukuu mwishoni mwa ziara yake ya siku Mbili Mkoa wa Kusini Unguja kuangalia Miradi ya Maendeleo.
  Balozi Seif akiikagua Bara bara ya Koani hadi Jumbi yenye urefu wa Kilomita 6.0 inayojengwa na Kampuni ya Mecco ili kuwaondoshea shida ya usafiri wananchi wa maeneo yanayopita bara bara hiyo
 Mhandisi wa Kampuni ya Mecco Bwana Nassor Ramadhan akimuahidi Balozi Seif kukamilishwa kwa Bara bara ya Koani Jumbi ndani ya Miezi Mitatu iwapo Mvua kubwa zitakatika kipindi hichi.

 Balozi Seif akishuhudia kasi ya maji safi na salama yanayotiririka katika Kisima cha Bambi kinachotarajiwa kupelekea huduma hiyo kwa wananchi wa Kijiji cha Uroa waliokosa huduma hiyo kwa muda mrefu.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Uroa kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu wa kukosa huduma za maji ambazo karibu zitakuwa Historia.
Balozi Seif akizungumza na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Mkutano wa Majumuisho ya ziara yake ya siku mbili Mkoani humo uliofanyika katika Ukumbi wa chuo Kikuu cha Taifa {SUZA} hpo Tunguu.


Na Othman Khamis, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wananchi wanapaswa kuendelea kujitolea na kuvumilia kutokana na changamoto zinazojitokeza kwenye Miradi ya Serikali  inayowagusa moja kwa moja ambayo imelenga kuwaletea Maendeleo.
Alisema kitendo cha baadhi ya Wananchi kubeba bango la kulalamikia vipando vyao katika kudai fidia licha ya kwamba ni haki yao lakini ile Miradi inayotekelezwa na kufikishia kwenye maeneo yao huleta faida na ustawi wa Maisha yao ya kila siku.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo akikamilisha ziara yake ya siku Mbili ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja alipokuwa akikagua maendeleo ya Miradi mbali mbali ya Maendeleo inayowagusa  Wananchi katika Shehia na Majimbo yao ikiwemo pia ile ya Chama cha Mapinduzi.
Alisema ipo miradi ya huduma za Maji safi na salama, ujenzi wa  Bara bara inayotekelezwa na Serikali Kuu ikiungwa mkono na Washirika wa Maendeleo miradi ambayo wakati mwengine vipando, mali pamoja na baadhi ya Nyumba za Wananchi hulazimika kuathirika kutokana na upanuzi wake mazingira ambayo Wananchi wanaopatwa na changamoto hiyo wanastahiki kuivumilia Serikali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi mbali mbali Nchini wanaoendelea kuwa wastahamilivu kutokana na athari hizo na kuwaahidi kwamba Serikali Kuu kupitia Taasisi zinazohusika na Miradi hiyo hazitaacha kuendelea kufanya Tathmini ya hasara zinazowakumba baadhi ya Wananchi hao kwa kupisha Miradi ya Ujenzi.
Akitoa Taarifa ya maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara ya Koani hadi Jumbi yenye urefu wa Kilomita 6.3 inayotarajiwa kujengwa katika kiwango cha Lami Mhandisi wa Ujenzi wa Bara bara hiyo kutoka Kampuni ya Mecco Bwana Nassor  Ramadhan alisema muendelezo wa Mradi huo umesita kutokana na Mvua kubwa zinazonyesha.
Mhandisi Nassor alisema Mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 40% baada ya kukamilika kwa kazi za usafishaji wa eneo linalopita Bara bara, kumwaga Vifusi pamoja na  uwekaji wa  Makalvati kwenye maeneo yanayopita maji.
Aliwahakikishia Wananchi wa vijiji vinavyopita bara bara hiyo kwamba ukamilishaji wa Mradi huo kwa sasa umebakisha Miezi Mitatu iwapo hakutakuwa na muendelezo wa mvua.
Mapema Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mheshimwa Ayoub Mohamed Mahmoud  alimuagiza Mhandisi wa Ujenzi wa Bara hiyo kuhakikisha kwamba anajenga mazingira ya haraka katika kipindi hichi cha mpito kuwawezesha Wananchi wanaotumia Bara bara hiyo wanaondokane na tatizo la usafiri wakati huu.
Mh. Ayoub alirejea kusema kwamba hatosita kufuatilia ahadi ya mkandarasi huyo ya kumwaga kifusi cha dharura kuanzia leo ili kuwapa fursa wananchi wanaotumia Mawasiliano hayo waweze kufika salama kwenye huduma za Afya pamoja na Wanafunzi kwenda na kurudi Skulini.
Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Uroa mara baada ya kukikagua Kisima cha Maji Safi na Salama kilichopo Kijiji cha Bambi ambacho kinatarajiwa kusambaza Huduma hiyo katika Kijiji chao Balozi Seif aliwapongeza kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu uliopelekea Serikali kukiona kilio chao.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika kuwasogezea Wananchi huduma muhimu ikiwa ni kukamilisha ahadi iliyotoa.
Aliwakumbusha Wananchi wa Bambi na Uroa pamoja na maeneo mengine Nchini kuendelea kupanda miti kwa wingi  ili lengo la kuvitunza vianzio vya Maji vinavyopelekea kupatikana kwa huduma ya maji salama ifanikiwe na hiyo ndio itakayothibitisha Jamii kubakia kuwa na Afya njema.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alimalizia ziara yake kwa kukagua Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Sayansi katika Kijiji cha Unguja Ukuu itakayofaidisha Wanafunzi wa Skuli ya jirani zinazoizunguuka Skuli hiyo.
Akizungumza na Wanafunzi wa Skuli hiyo Balozi Seif  alisema Serikali Kuu imekuwa ikitumia gharama kubwa kuwajengea mazingira bora ya Kielimu Wanafunzi hao wanaolazimika kuitumia vyema fursa hiyo katika kujifunza Taaluma.
Balozi Seif alisema Kijana kamwe hataweza kufikia kiwango cha kuwa Mtaalamu kama hakujitayarisha kubobea katika fani ya Sayansi ambayo kwa sasa ndio inayouzika na kukubalika kutoa ajira katika Taasisi, mashirika ya Umma na hata Sekta Binafsi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea faraja yake na kusema inapendeza kuona ufaulu wa Wanafunzi wa Kike katika ngazi ya Sekondari inaongezeka kila Mwaka jambo ambalo ametoa tahadhari kwa Wanafunzi wa Kiume walazimike kukaza kamba vyenginevyo wanaweza kujikuta walezi wa Nyumba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.