Habari za Punde

Serikali yavunja Mkataba na Mkandarasi Ujenzi wa Jengo la Polisi Manyara

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu) akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi  baada ya kuwasili leo kwa ziara ya kikazi huku akitoa taarifa ya Serikali kuvunja Mkataba na Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi la  Polisi mkoani Manyara  lengo ni kuepuka gharama za ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Manyara baada ya kuwasili leo kwa ziara ya kikazi huku akitoa taarifa ya Serikali kuvunja Mkataba na Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi la  Polisi mkoani hapo lengo ni kuepuka gharama za ujenzi huo.Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Babati Mjini,Pauline Gekul.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Cyprian Mushi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu),wakati wa ziara ya Ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofis za Polisi mkoani hapo
Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),baada ya kumaliza Kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Manyara juu ya Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Jeshi la Polisi mkoani hapo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.