Habari za Punde

OFISI YA MTAKWIMU YAFANYA WARSHA KWA WAKURUGENZI MIPANGO NA SERA

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Mkurugenzi wa Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Mtakwimu wa Serikali Bi Khadija Khamis Hamad amesema licha ya juhudi zinazochukuliwa na serikali ya kukusanya takwimu rasmi katika kupanga malengo iliyojiwekea bado kuna mapungufu ya kukamilika kwa takwimu hizo nchini.
Bi Khadija ameyasema hayo wakati akifunga warsha ya siku moja  kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu huko Mazizini kwa Wakurugenzi Mipango,Sera na Utafiti wa Taasisi mbalimbali za serikali amesema ikiwa ni shamra shamra ya Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, Ofisi ya Mtakwimu inahitaji juhudi za ziada kupata takwimu rasmi ili kukidhi mahitaji ya takwimu hizo kwa watumiaji  .
Ameeleza kuwa kuna taarifa nyingi za kitaifa na kimataifa ambazo zinahitaji takwimu rasmi ili kupima utekelezaji wake hivyo ofisi ya Mtakwimu Mkuu pekee haiwezi kukidhi mahitaji ya mipango hiyo kwa kutoa takwimu hizo rasmi  
Amezitaja juhudi hizo ni pamoja na kuweza kutumia takwimu zisizo rasmi na kuzigeuza kuwa rasmi ili ziweze kupunguza au kuziba pengo liliopo katika mahitaji ya takwimu.
Aidha amefahamisha kuwa takwimu rasmi ni takwimu ambazo zinaratibiwa na kufuata miongozo ya Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ambae ndio mtoaji pekee wa takwimu rasmi za serikali.
Ameeleza kuwa changamoto iliopo ni jinsi ya kuweza kuzipata takwimu hizo zisizo rasmi na kuweza kuziunganisha na takwimu rasmi kutokana na kutofautiana kwa njia ya ukusanyaji wake.
“Tunafahamu kwamba asasi za kiraia zinafanya tafiti nyingi ambazo zinaweza kuziba mapengo ya takwimu zinazokosekana lakini tafiti hizo hazitambuliani na Ofsi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa sababu hazikufuata utaratibu wa kuwa takwimu rasmi”, alieleza Mkurugenzi huyo.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema lengo la warsha hiyo ni kukutana na wadau wa wakuu wa takwimu, wazalishaji na watumiaji ili kujadiliana changamoto ambazo Ofisis ya mtakwimu Mkuu inazikabili katika upatikanaji wa takwimu rasmi na namna ya kuzigeuza kuwa ni fursa katika utekelezaji.
Nae Mwezeshaji Asya Hassan Mussa kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali amesema takwimu hukusanywa kwa kutumia dodoso ambazo hupelekwa katika taasisi kwa ajili ya kupata kiwango cha viashiria vya takwimu  ili kupata idadi ya takwimu hizo lakini changamoto iliopo ni kutokamilika kwa dodoso hizowakati wanapozifuata na kupelekea kutopata takwimu rasmi.
Nao washiriki wa warsha hiyo wameiomba jamii, taasisi za serikali na binafsi kutoa takwimu zenye uhalisa wa jambo ili kuweza kufanikiwa kwa kupata takwimu rasmi kwa lengo la kufikia malengo yalijiwekea serikali na kuleta maendeleo nchini
Warsha hiyo ni ya siku moja ambapo mada mbalimbali zilijadiliwa ikwemo Uzowefu wa Ukusanyaji wa Takwimu rasmi na Ukusanyaji wa Takwimu katika Wizara, Idara na Mashirika ambapo Ujumbe wa Mwaka huu ni “kilammoja anahusika: Takwimu zenye ubora ni muhimu katika kuhakikisha usimamizi mzuri wa uahamaji wa lazima katika Bara laAfika”.

        

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.