Habari za Punde

Wawekezaji wa Mahoteli Kufuata Muongozi na Sheria

 
Meneja wa Uwezeshaji na Maendeleo ya Mradi wa (ZIPA) Ndg. Othman Maulid Suleiman akimsomea maelezo ya tamko la Serikali  Meneja Mkaazi wa Hoteli   Moh’d Yussuf Mbamba wa Emerau Bay Resort Hoteli mbele ya wajumbe wa taasisi mbalimbali za Serikali wakati walipofanyiwa ukaguzi Hotelini hapo. 
Meneja Mkaazi wa Hoteli Moh’d Yussuf Mbamba wa Emerau Bay Resort Hoteli akitia sainitamko la Serikali  baada ya kusomewa maelezo mbele ya wajumbe wa taasisi mbalimbali za Serikali wakati walipofanyiwa ukaguzi Hotelini hapo.
Meneja wa Uwezeshaji na Maendeleo ya Mradi wa (ZIPA)   Othman Maulid Suleiman  na Memeja wa Hoeti ya Misali Sunset Beach Zahran Juma Ali wakisaini maelezo ya tamko la Serikali wakati walipofanyiwa ukaguzi mara walipofika katika Hoteli hiyo.

Na. Miza Othman – Maelezo Pemba. 
Waekezaji wa Hoteli wametakiwa kuzifuata Sheria na muungozo  ulioekwa na Serikali ili kuondokana na migogoro isyokuwa ya lazima.

Aliyaeleza hayo Memeja wa Uwezeshaji na Maendeleo ya Mradi wa (ZIPA)   Othman Maulid Suleiman katika Hoteli tofauti zilizotembelewa na Wajumbe wa Kamati za Taasisi za Serikali  kwa ajili ya kukagua Miradi yao.
Alisema  lengo la Serikali ni kuwakumbusha waekezaji hao ili kufuata  taratibu na kusaini tamko kutoka Serikalini kwani inania  thabiti ya kuendeleza Uchumi  kati ya Nchi na Wawekezaji hao.
Aidha alisema wamiliki wa Hoteli ni lazima wawe huru katika maeneo waliyoekeza kwani maeneo hayo yamemilikiwa na  Serikali.
“Wamiliki ni lazima wawe hurunkatika maeneo walioekeza kwani Ardhi ni mali ya Serikali”,alisema Meneja Othman Maulid.
Hata hivyo aliwataka wafanya kazi wa Hoteli hizo kuwa wazalendo katika Nchi yao wakati watumishi kutoka taasisi za Serikali wanapohitaji taarifa  za maendeleo ya waekezaji  hao.
 Nae Meneja wa Idara ya Uwezeshaji na Maendeleo ya Mradi kutoka Pemba (ZIPA)  Ali Shaaban Suleiman alisema lengo la ziyara hiyo ni  kuwapatia maelezo  yaliyoandaliwa ili kuwakumbusha Wawekazaji hao.
Pia  aliwataka wawekezaji hao kutofanya makubaliyano ya kienyeji na wananchi wa shehiya hilizokaribu nao ni vyema kukimbilia katika vyombo husika ili kuondoa changamoto zinazowakabili baina yao na wananchi hao.
Kwaupande wao Waekezaji hao wamesema watawaachi huru wananchi wanaojishughulisha na Shughuli za  uvuvi kwani na wao hujitafutia riziki katika kujiendeleza kimaisha.
Hata hivyo Wawekezaji  hao wamewaomba Wajumbe wa Kamati hiyo kuwafikishia sehemu husika suala zima la kimavazi linalichafua utamaduni wa Mzanzibar na kuwataka watembezaji wageni kutafutiwa vitambulisho maalum kwani kufanya hivyo kutaepusha  uhalifu usiokuwa walzaima.
Pia Wawekezaji hao wamewashukuru Wajumbe wa Kamati hiyo kwa kuchukua uwamuzi wa kuwakumbusha na wameahidi kuyafanyia kazi kama walivyoelekezwa.
Jumla ya Hoteli 5 za Mkoa wa Kusini Pemba zilifanyiwa ukaguzi ikiwemo Fundu Lagoon, Emerau bay Resort, Misali Sunset Beach, Annex Pemba Isla Hotel na Archipelago Hotel.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.