Habari za Punde

TANESCO KWA MARA YA TATU YAWA MSHINDI WA KWANZA KATIKA TUZO ZA UBORA KATIKA UANDAAJI WA TAARIFA ZA FEDHA KWA TAASISI ZA UMMA


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha  ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Bi.Renatha Ndege katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za umma na binafsi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Desemba 7, 2019.

Na. Mwandishi Wetu.
SHIRIKA la Umeme nchini Tanzania, TANESCO limeshika nafasi ya kwanza na kunyakua tuzo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha  ya Mwaka 2018 (Best Presented Financial Statements for the Year 2018 Awards) inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.Amina Khamis Shaaban amemkabidhi tuzo hiyo Afisa Mkuu wa Fedha (CFO) wa TANESCO, Bi. Renatha Ndege katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za umma na binafsi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Desemba 7, 2019.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Renatha alisema, TANESCO imetwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

“Sisi kama Shirika tumefurahi sana, huu ni ushindi mkubwa, ili upate tuzo hii, kuna vigezo vinavyotumika na kubwa kuliko yote lazima uwe na hati safi, hii inamaanisha kwamba hela za Watanzania ziko salama.” Alisema.

Aliishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kuendelea kuliamini Shirika pamoja na Wizara kwa kutoa fedha nyingi kujenga miradi mingi na mikubwa ya uzalishaji umeme.

“Kama mnavyoona miradi ya umeme ni mingi Shirika liko salama, na hivi sasa umeme ni wa uhakika, hii inamaanisha kuna mambo mazuri yako TANESCO.” Alisisitiza.

Aliipongeza timu nzima ya idara ya Uhasibu na ukaguzi TANESCO kwa kufanya kazi nzuri iliyo pelekea Shirika kupata ushindi huu mkubwa.
 Bi.Renatha Ndege, akiwa amebeba tuzo hiyo, huku akisindikizwa na watumishi katika idara yake wakati wa hafla hiyo.
 Bi.Renatha Ndege, akiwa amebeba tuzo hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa na tuzo hiyo.
 Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa na tuzo hiyo wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi.Amina Khamis Shaaban, akitoa hotuba yake.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Meza kuu.
 Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Profesa Isaya Jairo, akitoa hotuba yake.
 Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Bw. Pius Maneno, akitoa hotuba yake.
  Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja ya washindi wa tuzo wakiwa na mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.