Habari za Punde

Vijana wa Vikundi vya Vijana Wilayani Chato Wakabidhiwa Hundi ya Mkopo ya Milioni 92.

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani (kulia) akicheza na kikundi cha vijana walipokuwa wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akihutubia vijana wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Mkopo wa Shilingi Milioni 92 kwa vikundi vya Vijana Wilayani Chato.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani akieleza jambo wakati wa hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akieleza jambo wakati hafla hiyo ya kukabidhi hundi ya Mkopo wa Shilingi Milioni 92 kwa vikundi vya Vijana Wilayani Chato.
Baadhi ya Vijana kutoka Geita, Chato na Bukombe wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akifafanua jambo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya Mkopo wa Shilingi Milioni 92 kwa vikundi vya Vijana Wilayani Chato.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani (kulia). Katikati ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Chato Bw. Christian Manunga.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.