Na.Miza Othman -Maelezo Pemba.
Mkurugezi Kilimo,Maliasili na Mazingira Baraza la Mji Chake-chake.Bi. Salma Abuu Hamad amewataka wajasiriamali wanaojishughulisha ufugaji wa kuku kubuni mbini endelevu ili kuondokana na utegemezi wa maisha.
Amesema ikiwa wafugaji hao watazifuwata taratibu na mbinu za fugaji kupitia kwa wataalamu wataweza kupiga hatua na kufikia malengo waliyokusudia sambamba na kutoa ajira kwa wengine.
Hayo yameelezwa na Msaidizi Mkurugenzi Kilimo, Maliasili na Mazingira.Ndg. Salum Zubeir Masiku kwa niaba ya Mkurugenzi alipokua akifungua Mafunzo ya Siku moja katika Ukumbi wa Mikutano Baraza la Mji Chake-chake alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka wajasiriamali hao kujipanga na kuunda vikundi vya ushirika kwani kufanya hivyo kutaweza kuwarahisishia upatikanaji wa mafunzo ya mara kwa mara na fursa nyengine zinapotokea badala ya mtu mmoja mmoja.
Hata hivyo amewaambia wajasiriamali hao fursa waliyoipata ni yapekee pia watakuwa wajumbe kwa wenzao kutokana na Elimu watakayopatiwa ni mbinu bora zitakazo wasaidia katika ufugaji wao.
“Kunabaadhi ya watu wamejiekeza katika mifugo wamejiajiri ,kuwapatia elimu watoto wao na hata wao kujiendeleza kimaisha katika jamii zao”, alisema Msaidizi Mkurugenzi Salum Zubeir.
Muezeshaji Mifugo kutoka Idara ya Mifugo Pemba Mohammed Ali Massoud amesema ni vyema kwa mfugaji kuwa na malengo katika ufugaji kwani kufanya hivyo ndiyo yatakayo muezesha kujikwamua kimaisha na kuongeza kipato ndani ya Nchi.
Hata hivyo Dkt. Mohammed Ali amewataka wajasiriamali hao wanaojishughulisha ufugaji wa kuku kuandaa maeneo maaluu yenye ubora ili kuiepusha mifugo yao na maradhi yanayoweza kuepukika katika mabanda yao ikiwemo mavumbi na hata upitishaji wa hewa katika mabanda hayo.
Aliwasisitiza kwa kusema wafugaji hao ni vyema kuwatafutia Kuku wao chakula chenye mchanganyiko ili kuwapatia makuzi yaliyobora ikiwemo Mtama, Dagaakavu na Muhundi na kuweza kupata wateja kwaharaka.
Nao wafugaji hao wamewaomba madaktari wa mifugo kuwa karibu nao katika kuzitatua chanagamoto zinazowakabili katika ufugaji wa kuku ikiwemo maradhi na sambamba na kuwaongezea taaluma zaidi ya ufugaji bora.
No comments:
Post a Comment