Habari za Punde

Wamiliki wa Mahoteli Watakiwa Kuheshimu Sheria za Kazi.

Na Miza Othman – Maelezo Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.Mhe. Omar Khamis Othman ametaka wamiliki wa Hoteli kufuata Sheria na  Utaratibu uliowekwa ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima baina yao na Serikali.
Aliyasema hayo wakati akipokuwa akizungumza na Wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali  juu ya uwajibikaji na kuheshimu muongozo wa utekelezaji wa  majukumu yao huko katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa .
Hata hivyo amewataka wajumbe hao kutofanya kazi kwa mazowea ili kuepusha muhali  kwa wamiliki wa Hotel  hizo kwani kufanya hivyo kutapelekea kuzotesha maendeleo ya Serikali katika Nchi yao.
“Watu wote ni watalii ikiwa Mweupe au mweusi tusidharau kitu twende kwa pamoja ili Zanzibar iwesalama”, alisema Mkuu wa Mkoa Omar Kahamis.
Aidha wamiliki wa Hoteli wametakiwa kuheshimu watu wote kwani kufanya hivyo ni kuzipahadhi Hoteli zao na pata wateja kwa urahisi ili kuingiza kipato kwa haraka na kuweza kuondoa changamoto zinazo wakbili katika kazi zao.
Nae Mukurugenzi kutoka Idara ya Uwezeshaji na Maendeleo ya Mradi (ZIPA) Shariff Ali Shariff  amesema lengo na madhumuni ni kuwakumbusha wamiliki wa Hoteli kuzifuwata sheria za kazi katika Utekelezaji wa majukumu yao ili kuondokana na chanagamoto zisizokuwa za lazima baina  ya Hoteli  na Serikali.
Pia Mkurugenzi huyo amesema Serikali ipo katika kutekeleza na  kusimamia majukumu yake bali si kuwaonea wamiliki wa hoteli hizo.
 “Nilazima Wajumbe wote wafuwate utaratibu na muongozo uliyoekwa ili kukamilisha lengo walilokusudia katika utekelezaji wa kazi yao”,  Alisema Mkurugenzi Shariffu Ali.
Wajumbe walioshiriki katika Mkutano huo  wamesema nilazima watumie gharama na kuchagua  watu madhubuti ili kuweza kupata taarifa za kila siku sio kutegemea wamiliki wa Hoteli kwani wanaweza kuwatumia taarifa zisizo za uhakika.
Hata hivyo wajumbe hao wamesema ni lazima wapewe nguvu na Viongozi wao ili kuweza kufanya kazi kwa uzalendo na sio kwa mazoea kwani kufanya hivyo kutapelekea kukamilisha kwa urahisi.
“ Watu wawe siriasi katika kutekelea majukumu yao na sio kuoneana umhali’, walisema wajumbe hao.
Jumla ya Hoteli 9n zitatembelewa na wajumbe ulioandaliwa na Serikali ili kujua sharia zinazofuatwa katika Hoteli hizo.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.