Habari za Punde

Kamati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Kusiomamia Ofisi za Viongozi na Wakuu wa Kitaifa Watembelea Miradi ya Nyumba za Maafa Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba.

OFISA Mdhamini Pemba Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Ali Salum Matta, aakiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa ofisi hiyo katika kipindi cha miezi sita Julai- Disemba 2019, kwa kamati ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi Zanzibar. 
WATENDAJI wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba, wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Taarifa ya utekelezaji wa ofisi hiyo katika kipindi cha miezi sita Julai- Disemba 2019, kwa kamati ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi Zanzibar. 
MWENYEKITI wa kamati ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi Zanzibar, Ali Suleiman Ali (Shihata) akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba, mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa Ofisi hiyo kwa wajumbe wa kamati hiyo.
MWENYEKITI wa kamati ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa ya Baraza la wawakilishi Zanzibar, Ali Suleiman Ali (Shihata) akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba 30 za maafa Tumbe Wilaya ya Micheweni
(PICHA NA ABDI SULEIMAN) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.