Habari za Punde

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Akitangaza Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri Yaliofanywa na Rais Dkt.John Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza  mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 23, 2020.

Katika mabadiliko hayo yaliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteuwa Mhe. Mussa Azzan Zungu  kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira 
Rais Magufuli amemteuwa Mhe, Goerge Simbachaweni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, anachukua nafasi iliokuwa ya Mhe. Kangi Lugola.
Pia ametengua uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thomas Andengenye  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.