Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein Afanya Uteuzi wa Viongozi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:

1. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO 
i. Bwana Iddi Haji Makame ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) katika Wizara ya Fedha na Mipango.

ii. Bwana Khatib Mwadini Khatib ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango.

iii. Dkt. Suleiman Simai Msaraka ameteuliwa kuwa Kamishna wa Bajeti katika Wizara ya Fedha na Mipango.

iv. Bwana Ame Burhan Shadhil ameteuliwa kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali katika Wizara ya Fedha na Mipango.

2. WIZARA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

i. Bibi Asha Zahran Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mifugo katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.

3. WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

i. Bibi Rahima Ali Bakari ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) katika Wizara ya Biashara na Viwanda. 

4. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

i. Bwana Mohamed Habib Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji  katika Kamisheni ya Ardhi.  

ii. Bwana Mtambua Hamziji Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ardhi katika Kamisheni ya Ardhi.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 5 Februari 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.