Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Azungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  katika kikao cha Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo mbili Julai-Disemba2019  kilichofanyika leo katika ukumbi Ikulu Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee (kulia) alipokuwa akiuliza suala katika  kikao cha  Utekelezaji wa mpango kazi wa kipindi cha robo mbili Julai-Disemba 2019 cha  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar (katikati) Waziri wa Elim na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma na Naibu Waziri Simai Mohamed Said (kushoto)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) akimsikiliza Naibu Waziri wa  Elimu na Mafunzo ya Amali Simai Mohamed Said (kuishoto) akichangia katika kikao cha  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo mbili Julai-Disemba 2019 cha Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, Mwenyekiti wake la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto),Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (wa pili kulia)
Mkurugenzi wa Maktaba Kuu Zanzibar Sichana Haji Foum alipokuwa akisisitiza jambo wakati  akichangia katika kikao cha Utekelezaji wa mpango kazi kwa kipindi cha Julai-Disemba 2019 cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Baadhi ya Maafisa katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara hiyo leo katika kikao cha  siku moja cha Utekelezaji mpango kazi kwa kipindi cha robo mbili Julai-Disemba 2019 kilichofanyika  Ukumbi wa Ikulu Mjini zanzibar
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Maalim Abdalla Mzee (kulia)  alipokuwa  akisoma taarifa ya Utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha robo mbili Julai-Disemba 2019 katika  kikao cha Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo  katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)Mkurugenzi Idara ya Mipango,Sera na Utafiti Khalid Waziri,(kulia). 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.