Habari za Punde

Zantel Yazindua Bonga MpakaBasi Kuwawezesha Wateja Kupiga Simu Mitandao Yote kwa Gharama Nafuu

Mkuu wa Biashara wa Zantel, Aneth Muga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Kifurushi chaBongaMpakabasikinachowawezesha wateja wa Zantel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama nafuu.Kushoto ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa.
Mkuu wa Biashara wa Zantel, Aneth Muga akionyesha Menyu ya *149*15#iliyoboreshwa zaidi ili kuwasaidia wateja kununua vifurushi kwa haraka zaidi.Maboresho hayo ni sehemu ya uzinduzi wa kifurushi cha ‘BongaMkapabasi’kinachowapa wateja uhuru wa kupiga simu mitandao yote kwa gharama nafuu.
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa akimulekeza Abdillahi Wadi Nahoda jinsi ya kujiunga na kifurushi chaBongaMpakabasikinachowawezesha wateja wa Zantel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama nafuu hapa nchini.Huduma hiyo imelenga katika kuboresha huduma za mawasiliano kwa wateja wote Visiwani na Bara.

Katika kuleta unafuu wa huduma za mawasiliano nchini, Kampuni ya simu ya Zantel imezindua bidhaa ya bando ijulikanayo kama ‘BongaMpakaBasi’ili kuwawezesha wateja wake kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama nafuu.
Huduma hiyo, itawafanya wateja wa Zantel kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa gharama ileile ya kupiga ndani ya mtandao kupitia kifurushi kimoja cha ‘BongaMpakaBasi’.Bidhaa hiyo inatajwa kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Biashara wa Zantel, Aneth Muga alisema bidhaa hiyo imelenga kuboresha huduma za mawasiliano na kuhakikisha wateja wanapata mawasiliano ya uhakika na kwa gharama nafuu hasa wanapopiga simu kwenda nje ya mtandao.

“Zantel tunatambua kuwa huduma za mawasiliano hasa za sauti na data ni huduma muhimu katika kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwakuwa watu wengi hutegemea mawasiliano ili kufanya shughuli za kila siku hasa biashara, kupata huduma za kijamii kama afya, malazi pamoja na usafiri,” alisema Muga.

Awali, Zantel ilikuwa na vifurushi vya aina mbili ikiwamo kifurushi cha kupiga simu ndani ya mtandao kilichoitwa ‘Bonga’ na cha mitandao yote maarufu kama ‘MpakaBasi’.Kwa sasa mteja wa Zantel atajiunga kifurushi kimoja cha BongaMpakaBasi na kuwasiliana mitandao yote kwa gharama ileile.

“Kwa sasa wateja wa Zantel wataweza kupiga simu kwenda mitandao yote ndani ya Tanzania bila kuhofia gharama au aina ya kifurushi ambacho mteja amejiunga.Vilevile, tumeboresha vifurushi vyetu pamoja na menyu ili kuwawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi na haraka zaidi,” alisema Muga. 
Pia, kupitia huduma hii Zantel inatekeleza mkakati wake wa kuhakikisha inawafikisha huduma kwa watu wengi zaidi na kuhakikisha inachochea maendeleo ya watu kupitia huduma bora za mawasiliano.

Naye, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed  Mussa alisema kampuni hiyo imeendelea kufanya uwekezaji kwenye miundombinu ya mawasiliano Visiwani Zanzibar, ambako ni eneo kitovu cha biashara kwa Zantel kwa lengo la kuboresha huduma za mawasiliano.

Uwekezaji huo umefanyika kupitia teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuweza kutoa huduma za sauti na data kwa kampuni nyingine za simu hapa nchini.

“Huduma bora za mawasiliano ni moja ya nguzo muhimu kwa maendeleo ya kila jamii. Mtandao wa 4G+ wa Zantel utachangia katika kuleta maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwamo elimu, fedha na afya pamoja na kuchochea ukuaji wa shughuli za uchumi na biashara,” alisema Mussa.
Ili kupata huduma hiyo mteja wa Zantel anaweza kupiga *149*15# na kuchagua BongaMpakaBasiili kujipatia vifurushi vya siku, wiki na mwezi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.