Habari za Punde

IGP SIRRO ZIARA YA UKAGUZI KILIMANJARO

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akikagua eneo la uwanja wa mbinu za medani lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, leo 06/03/2020, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (wapili kulia) akitumia darubini kuangali wakati alipofanya ziara ya ukaguzi eneo la uwanja wa mbinu za medani lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, leo 06/03/2020, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akizungumza na maofisa wa vyeo mbalimbali (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika Shule ya Polisi Moshi iliyopo mkoani Kilimanjaro, leo kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Hamduni na kushoto ni Kaimu Mkuu wa shule hiyo ya Polisi ACP Omar K. Omar. Picha na Jeshi la Polisi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.