Habari za Punde

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YAIPONGEZA WAKALA WA VIPIMO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege (aliyenyoosha mkono)  akiwaongoza wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira waliofika kutembelea katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani kujionea shughuli zinazofanywa ikiwemo kujifunza mambo mbali mbali.
Mjumbe wa kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira akiuliza swali mara baada ya  mara baada ya katika kituo Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero (aliyenyoosha mikono) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Vipimo Kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani, Alban Kihuld (wa tatu toka kushoto).
Wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira akitembelea katika kituo cha Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu Kibaha- Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero akieleza jambo kwa vyombo vya habari mara baada ya kupata maelezo juu ya utendaji kazi na majukumu ya Wakala wa Vipimo mara baada ya katika kituo cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege akiongea na wanahabari juu ya huduma zinazotolewa na wakala wa vipimo mara baada ya kutembelewa na wabunge kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira katika kituo chao cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imewapongeza Wakala wa Vipimo (WMA)kwa kufanya kazi kisasa ili kuendana na sera ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq amewataka kuendelea kujituma kwa kufata sheria na taratibu za upimaji.

“Kiukweli nimefurahi kufika mahali hapa na kujionea mambo mengi yanayofanywa kisasa na wakala wa Vipimo katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani hivyo niwaombe waendelee kuchapa kazi kwa bidii," amesema Mhe. Saddiq.

Ameongeza kuwa Wakala wa Vipimo wamekuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto hasa katika upimaji magari na upimaji wa mita za maji na kuziomba mamlaka za maji ikiwemo DAWASA,DUWASA, MURUWASA lazima zote zipitie hapa WMA na kuhakikiwa kisha kupewa kibari tayari kutumika kwenye jamii.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege, amesema mafanikio ya kituo hicho yametokana na kujituma na kupata ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini kwa kutatua baadhi ya changamoto.

Amesema mpaka sasa kituo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuendelea kusimamia misingi na kanuni bora katika upimaji wa matenki ya mafuta na dira za maji. "Tumepewa dhamana ya kuhakikisha matenki ya mafuta yana hakikiwa hapa, yanapoenda kujazwa mafuta, na Dira za Maji zinazoletwa nchini zote lazima zipimwe ili kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mita sahihi” amesema Ludovick.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.